Watetezi wa haki katika wilaya ya Australian Capital Territory wamesema uamuzi wa serikali ya wilaya hiyo kuongeza umri wa uwajibikaji wa uhalifu, unastahili kuwa mfano kwa majimbo na wilaya zingine. A-C-T imekuwa mamlaka yakwanza nchini Australia kuongeza umri ambapo mtoto anaweza wajibishwa kwa uhalifu akiwa na miaka 14.
Serikali ya Tanzania imekanusha vikali tuhuma zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na kudai kuwa zinaihusisha yenyewe na kiongozi wa upinzani, Tundu Antipas Lissu, katika mpango wa kumuwekea sumu mshtakiwa huyo. Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Julai 3, 2025, na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Serikali imetoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa hizo, ikisisitiza kuwa "hazina ukweli wowote."
Watu sita waliodaiwa kuwa wachawi wameuawa kwa kupigwa, kuchomwa moto na kupigwa mawe katika kijiji cha Gasarara, kilomita chache kutoka jiji la Bujumbura, nchini Burundi. Mashuhuda wanasema shambulizi hilo lilitekelezwa na vijana wa kundi la Imbonerakure, linalohusishwa na chama tawala cha CNDD-FDD.