Kuna uwezekano wakaaji wa Tasmania wana weza elekea debeni hivi karibuni, kiongozi wa jimbo hilo Jeremy Rockliff akitarajiwa kufurushwa ofisini na bunge. Serikali hiyo ya wachache ya chama cha Liberal, inakabiliwa na machafuko yakisiasa baada ya Bw Rockliff kukabiliwa kwa kura yakutokuwa na imani dhidi yake jana Jumatano 4 Juni, mjadala mrefu unatarajiwa kuendelea vikao vitakapo anza tena leo asubuhi.
Polisi jijini Dar es Salaam Tanzania wamezingira jengo la kanisa la Ufufuo na Uzima linalomilikiwa na mbunge wa jimbo la Kawe Josephat Gwajima, ambaye wiki iliyopita, alilaani matukio ya utekaji nchini humo.
Wakati huu wakikabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi, raia wa Burundi ingawa wamechoka lakini wanajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa wabunge wa Juni 5 ambao umepoteza mvuto na kukosekana kwa washindani wa kweli.
Msafara wa Hija ume anza mjini Mecca, ambako zaidi ya idadi yawa Islamu milioni 1.5 kutoka duniani kote watawasili Saudi Arabia kutekeleza wajibu wao wakidini. Tukio hilo ni moja ya nguzo tano za Uislam, wajibu wa maramoja katika maisha kwa kila Muislamu anaye weza imudu, na ana uwezo kimwili wakufanya hivyo.