Kiongozi wa NSW Dominic Perrottet, atupilia mbali ukosoaji wa Waziri Mkuu Albanese, nakusisitiza ana amini chama chake cha NSW Liberals, kinastahili kuwa na awamu ya nne madarakani. Amesisitiza kuwa malengo yake ni kwa siku za usoni za jimbo hilo, si mashambulizi binafsi.
Serikali ya shirikisho imetoa data mpya inayo onesha maelfu yawazee nchini Australia, wamefaidi kupitia madawa ya bei nafuu pamoja naku waona ma GP, wakati mageuzi mapya yame anza kutumika. Mageuzi kwa vizingiti vya mapato kwa kadi ya afya ya shirikisho yawazee, mwezi Novemba ilipanua upatikanaji kwa wazee elfu 10,893. Vizingiti kwa watu wasio na wachumba vili inuliwa kutoka $58,000 hadi $90,000. kwa wachumba vizingiti viliongezeka kutoka $92,416 hadi $144,000.
Burundi ilitangaza Ijumaa kwamba ingepeleka wanajeshi 100 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuanzia Jumamosi, kama sehemu ya kikosi cha kikanda.
Afisa mkuu wa jeshi la Burundi aliliambia shirika la habari la AFP kwamba wanajeshi hao walikuwa tayari kuungana na wenzao wa nchi zingine za kikanda, katika operesheni hiyo. Baadhi ya mataifa saba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yalituma wanajeshi mwishoni mwa mwaka jana mashariki mwa DRC, eneo ambalo limekuwa likipambana na kuongezeka kwa wanamgambo, wakiwemo waasi wa M23.
Majimbo sita yanayoongozwa na upinzani nchini Nigeria yameiomba mahakama ya juu kutupilia mbali matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, wakisema chombo cha kusimamia uchaguzi kilivunja sheria na kanuni zake wakati wa kuhesabu kura, hati za mahakama zilionyesha. Mgombea wa chama tawala cha All Progressive Congress (APC) Bola Tinubu alitangazwa mshindi siku ya Jumatano, lakini wapinzani wawili kutoka vyama vikuu vya upinzani walisema matokeo hayo yalikuwa ya udanganyifu na kuapa kuyapinga mahakamani.