Taarifa ya Habari 6 Februari 2025

Bench - Swahili.jpg

Nchi zaki Arabu, Umoja wa Mataifa na washirika wakaribu wa Marekani wamekosoa pendekezo la Donald Trump kuchukua ukanda wa Gaza, naku tawanya wa Palestina kuwa hatua hiyo ita yumbisha kanda hiyo na kudhoufisha juhudi zakupata suluhu ya nchi mbili.


Upinzani wa shirikisho wakaribisha uamuzi wa serikali ya Labor ku unga mkono, adhabu ya chini ya lazima kwa baadhi ya makosa ya ugaidi na maonyesho ya alama za chuki.

Utabiri wa mvua kubwa katika mji wa Townsville, ume zua hofu kuhusu tisho za mafuriko wakati vikosi vya ulinzi wa taifa la Australia vinawasili mjini humo kutoa msaada. Mji wa Townsville, ume athiriwa zaidi kwa mafuriko katika wilaya ya Kaskazini Queensland. Wanajeshi wame wasili mjini humo kusaidia kukarabati daraja lililo vunjika kwa sababu ya hali hiyo ya hewa. Na idadi ya wafanyakazi wa dharura 300 wa ziada wamewasili mjini humo kutoa msaada.

Serikali ya muungano wa kitaifa ya Afrika Kusini inayumba yumba kutokana na tofauti kati ya vyama tanzu vinavyounda serikali, lakini rais Cyril Ramaphosa amesema serikali hiyo ni thabithi. Ramaphosa anatarajiwa kulihutubia taifa kesho Alhamisi kuhusu utendakazi wa serikali hiyo, kwa mara ya kwanza tangu ilipoundwa.

Shirika la kimataifa la Action AID pamoja na yale ya ndani nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, yanasema bei ya baadhi ya bidhaa kwenye mji wa Goma, imeongezeka maradufu wakati huu mzozo unaoendelea ukizuia misaada na usambazaji wa malighafi. Kwa mujibu wa ripoti hiyo pamoja na shuhuda za wakaazi wa mji wa Goma ni kuwa Bei ya baadhi ya vyakula muhimu imeongezeka tangu waasi wa M23 walipodai wanaudhibiti.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service