Australia ina zingatia kuruhusu kuingiza nchini nyama za ng'ombe za Marekani, inapotafuta kupata makubaliano kwa ushuru wa biashara ya Donald Trump. Hatua hiyo inafuata maombi kutoka uongozi wa Rais kabla ya mkutano wa Waziri Mkuu Anthony Albanese, na Bw Trump watakapo jadili uwezekano wa msamaha wa ushuru. Bw Albanese amesema kuingiza nchini nyama ya ng'ombe ya Marekani, kuta ruhusiwa tu kama haku athiri itifaki za kitaifa za usalama wa mimea na wanyama.
Ripoti mpya imedokeza kuwa uchovu wa watunzaji, una wagharimu wa Australia afya yao, taaluma na takriban $18,000 kila mwaka. Ripoti ya shirika la The Sandwich Generation kwa kundi la Australian Seniors, imepata watu tisa kati ya kumi (90%) hupitia uzoefu wa uchovu wakutoa utunzaji, wakitoa karibu masaa 30 kila wiki au masaa 1,500 kila mwaka, kwa utunzaji, hali inayo wakosesha muda wao binafsi. Shirika la The Sandwich Generation lina zungumzia watu ambao wanaweza kuwa watunzaji wa wazazi wao ambao wame zeeka na wajukuu wao pia.
Raia wa Burundi wanapiga kura katika uchaguzi wa bunge ambao hauna kitisho chochote baada ya chama kikuu cha upinzani kuzuiwa kugombea. Chama tawala cha CNDD-FDD cha Rais Evariste Ndayishimiye kinatuhumiwa kwa kuhujumu mpinzani wake mkuu, National Freedom Council - CNL, ambacho kilimaliza katika nafasi ya pili kwenye uchaguzi uliopita wa 2020 na kikadai kuwa matokeo yalichakachuliwa. Mnamo mwaka wa 2023, wizara ya mambo ya ndani ilikifungia chama cha CNL kuhusiana na kile ilichokiita "makosa" katika namna kilivyoandaa mikutano yake.
Nchini Kenya, mwanaharakati wa mtandaoni Rose Njeri aliachiliwa kwa dhamana mnamo Juni 3. Msanidi programu huyu alikamatwa Ijumaa, Mei 30, baada ya kuunda jukwaa la mtandaoni kuwezesha raia wa Kenya kueleza kutokubaliana kwao na Mswada wa Fedha wa mwaka 2026. Mnamo Juni 3, katika Mahakama ya Milimani jijini Nairobi, Rose Njeri alishtakiwa kwa "kuingilia mfumo wa kompyuta bila kibali," shtaka ambalo liko chini ya Sheria ya Uhalifu wa mtandaoni.