Seneta huru David Pocock ameomba muda wa makato ya kodi yamawese ongezwe.
Makato hayo ya muda ya senti 22 za kodi yamawese, yameratibiwa kuisha mwisho wa mwezi huu, serikali ya shirikisho ikisema hatua hiyo haiwezi ongezewa muda kwa sababu ya shinikizo za bajeti. Wakati huo huo Benki ya Hifadhi ime ongeza viwango vya riba kwa mwezi watano mtawalio. Kiwango cha hela taslim kimefikia 0.5% kwa mwaka wa saba nakufikia 2.35%.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameahidi kuhakikisha kwamba anakabidhi madaraka kwa uongozi mpya, wa Dr. William Ruto. Katika ujumbe uliorekodiwa na kuwekwa kwenye mtandao wa You Tube, Kenyatta hata hivyo ameonekana kukosoa uamuzi wa mahakama ya juu uliotupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa William Ruto. Kesi hiyo iliwasilishwa na Raila Odinga wa muungano wa Azimio. Mwenyekiti wa mrengo wa Azimio ni rais Uhuru Kenyatta.
Mataifa Tajiri yamesema yatatumia karibu dola bilioni 25 ifikapo mwaka wa 2025, ili kupiga jeki juhudi za Afrika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Mkutano wa kilele wa tabia nchi ulifanyika Rotterdam, Uholanzi.