Mazingira ya joto yame endelea kushuhudiwa katika sehemu nyingi za NSW leo jumanne, moto ukiendelea kuwaka na nyuzijoto zikiendelea kupita thelathini. Bado kuna visa kadhaa vya moto ambavyo havija dhibitiwa licha ya baadhi kama moto wa Tambaroora unao waka karibu ya Bowral, ambao kiwango chake kimepunguzwa kwa tazama nakuchukua hatua.
Mafuriko yame endelea kuathiri enoe la Wilaya ya Kaskazini, barabara na madaraja yakifungwa na wakaazi wakiendelea kuwa katika vituo vya uhamisho vya dharura. Mililita mia mbili ya mvua imenyesha kati ya miji ya Alice Springs na Darwin, na vifaa vya chakula vikisafirishwa kupitia barabara mbadala na angani.
Kukosekana kwa elimu ya afya ya uzazi na vifaa tiba katika hospitali za vijijini nchini Tanzania kumetajwa kuwa ni miongoni mwa changamoto zinazo wakabili wanawake kutohudhuria kliniki hali inayo pelekea kujifungulia majumbani.
Kundi la raia wa Kongo wenye asili ya kitutsi wamekuwa wakilindwa na polisi wenye silaha wakati wakijiandikisha kupiga kura katika mji wa Nyangezi ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku mmoja wao alilieleza kuwa kampeni za ghasia zimelenga kuwaengua katika uchaguzi ujao.