Jamii yawa Islamu wa Australia imezindua kampeni yakitaifa yakutoa damu, kwa lengo laku wasajili zaidi ya watu elfu moja katika jamii zote. Zaidi ya misikiti 40 kote nchini Autralia, imeweka vituo wikendi hii kama sehemu ya kampeni ya kila mwaka yakuchangisha hela, inayo ongozwa na shirika la matibabu lawa Islamu, pamoja na shirika la Msalaba mwekundi la Australia Lifeblood.
Mashambulizi na ghasia zimeripotiwa kote nchini Nigeria wakati raia walipokwenda kupiga kura kumchagua rais na viongozi wengine, licha ya mamlaka kupeleka vikosi vizito vya usalama . Nigeria yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika imekuwa ikijitahidi kutokomeza ghasia na kuboresha uchumi wake. Nigeria inachagua rais mpya na makamu rais, maseneta na wawakilishi wa bunge katika uchaguzi ambao unajumuisha wapiga kura milioni 93.
Maafisa wawili wa polisi wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulizi linaloshukiwa limefanywa na mwanamgambo wa al-Shabaab kwa gari ya polisi karibu na kambi ya wakimbizi ya Dadaab, kaskazini mashariki mwa Kenya. Maafisa wa usalama nchini Kenya wanasema maafisa wawili wa polisi wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa wakati gari waliyokuwa wakisafiria ilikanyaga kilipuzi kwenye barabara ya Garissa na Dadaab, katika kaunti ya Garissa.