Taarifa ya Habari

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mji wa Melbourne unatarajiwa kufungua hospitali ya kwanza nchini Australia inayotibu magonjwa ya moyo.


Hospitali hiyo itafanya upasuaji 2150 wa moyo, kutoa huduma za dharura kwa watu elfu 28,300 pamoja na kutoa huduma 108,000 kila mwaka. Hospitali hiyo pia itatoa huduma zamatibabu kwa simu kupunguza mahitaji ya wakaaji wa maeneo ya vijijini kusafiri kumwona mtaalam, pamoja nakutumiwa kuwafunza mamia yawanafunzi kila mwaka.

Zaidi ya nyumba elfu 60 na biashara ziliachwa bila umeme na mashindano ya boti yakimataifa kufutwa, baada ya dhoruba kali kugonga maeneo ya mji wa Sydney jioni ya Jumamosi. Juhudi zakufanya usafi ziliendelea leo Jumapili na zinatarajiwa kuendelea katika wiki ijayo. Upepo mkali wenye kasi ya kilomita 100 kwa saa, ulirekodiwa kote mjini humo.

Wiki moja baada kimbunga Gabrielle kugonga New Zealand [[Feb 12]], mamlaka wamethibitisha kuwa watu wawili wame uawa, hali ambayo imefikisha idadi ya vifo kuwa 11. Bado kuna maelfu ya watu ambao haijulikani waliko, hali inayo fikisha idadi hiyo kuwa 6,431.

Ripoti ya uchunguzi ya Amnesty International yaonesha namna ambavyo M23 waliwauwa wanaume na kuwabaka wanawake na wasichana Mashariki mwa DRC. Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International,limechapisha ripoti yake ya uchunguzi unaonesha huenda waasi wa M23 wamefanya uhalifu dhidi ya ubinaadamu Mashariki mwa Kongo. Ripoti hiyo inasema waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda waliwauwa wanaume na kuwabaka wanawake chungunzima mashariki mwa Kongo mwishoni mwa mwezi Novemba. Amnesty International inasema manusura wa ubakaji na mashambulizi mengine bado hawajapatiwa msaada wa kutosha.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari | SBS Swahili