Theluthi tatu yawa Aboriginal na wana visiwa wa Torres Strait ni wajukuu wa wahanga wa vizazi vilivyo ibiwa, na wengi wao wamechangia hadithi za familia zao pamoja na kumbukumbu zao zaku ondolewa wakiwa watoto.
Wiki ya upatanisho inapo anza, viongozi wa mataifa ya kwanza wanaomba kuwepo kwa mchakato wakusema ukweli, pamoja na hatua thabiti kutoka kwa wanasiasa kushughulikia hasara inayo endelea.
Katika ardhi ya kitamaduni ya watu wa Dharug wa Parramatta, magharibi Sydney... moja ya sherehe nyingi zilizo fanywa kote nchini, kuadhimisha hafla ya 28 ya siku ya Kitaifa yaku omba radhi, na kukumbuka historia ya vizazi vilivyo ibiwa.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.