Ripoti mpya kutoka Anglicare Australia imetoa mpango waku kabiliana na upatikanaji wa nyumba za bei nafuu katika muda wa miaka 20 ijayo, mpango huo ukiwa una husu mageuzi ya sera za serikali.
Kumiliki nyumba kume julikana kama "ndoto kubwa ya Australia". Ila, kama vile chunguzi kadhaa zime pata, kuna tatizo kwa gharama ya nyumba hizi kwa sasa.
Ripoti mpya ya Anglicare kwa nyumba za bei nafuu, inatoa mpango wakuondoka katika janga hili. Wanaomba jaribio la mifuno ya upangaji wa muda mrefu kwa nyumba binafsi zakukodi. Na ujenzi wote wa nyumba mpya zijumuishe nyumba za kodi nafuu.