Key Points
- Every state operates its own public transport network, so rules and rates differ
- Pre-paid smartcards are available in all major cities and payment options may include contactless bank card transactions
- Ticketing compliance and safety are checked by staff and the use of CCTV cameras in all transport networks
*Kadi ya kulipia kabla ya usafiri wa umma katika mji mnaoishi ni ipi?
*Je, mnatumiaje kadi ya kielektroniki?
*Je, mnaweza kulipa kwa kutumia kadi ya benki kwa usafiri wa umma nchini Australia?
*Je, maafisa walioidhinishwa wanaweza kukagua nini vituoni na ndani ya vyombo vya usafiri?
*Je, ni makosa gani baadhi yanayohusiana na usafiri wa umma?
*Ni nini kinachotokea ikiwa mtapata faini?
*Je, ni membe za usafiri wa umma nchini Australia?
*Je, mnatakiwa kuwa kimya wakati wa kutumia usafiri wa umma nchini Australia?
Je, usafiri wa umma unapatikana popote nchini Australia?
Waaustralia wengi husafiri kwa magari binafsi wanapoenda kazini. Ni takwimu zinazotolewa na Ofisi ya Takwimu ya Australia (ABS) tangu 1976, wakati walipoanza kuuliza swali hilo.
Profesa John Nelson ni Mwenyekiti wa Usafiri wa Umma katika Taasisi ya Mafunzo ya Usafiri na Usafirishaji ya Chuo Kikuu cha Sydney. Anasema, miji iliyosambaa ya Australia na umbali mkubwa kati ya miji, inafanya kuwa vigumu kuhudumia maeneo ya vijijini kwa usafiri wa umma. "Hata unaposafiri nje ya Sydney, utaona kwamba mali zinapojitokeza kuwa mbali mbali."
Lakini katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu na miji mikubwa, usafiri wa umma ni kwa njia nyingi haraka zaidi, gharama nafuu na hata muhimu kwa watumiaji wengine.

Je, ni kadi gani ya kulipia usafiri wa umma katika jiji mnaloishi?
Kila jimbo au eneo lina mtandao wake wa usafiri, huku miji mikuu na miji mikubwa ikitumia mfumo wa tiketi za kadi za kisasa kwa malipo bila pesa taslimu. Kadi ya awali ya kulipia inayotumika katika kila mji mkuu wa jimbo au eneo ni:
- Opal card for Sydney
- Myki for Melbourne
- go card for Brisbane
- SmartRider for Perth
- metroCARD for Adelaide
- GreenCard for Hobart
- Tap and Ride Card for Darwin
- MyWay for Canberra
Je, mnatumiaje kadi ya kidijitali?
Mifumo ya kadi za kidijitali kwa ujumla ni rahisi kutumia, anasema Prof Nelson.
Lakini ikiwa hamjawahi kuitumia hapo awali, haya ndiyo mnayohitaji kujua.
“Kwa kawaida ni ukubwa wa kadi ya benki, mnaiwekea thamani kabla na kuitumia kuingia kwenye mifumo ya usafiri wa umma, iwe ni basi, treni, tram au feri.”
Kuhusu jinsi ya kuitumia, kiashiria mara nyingi ni kwenye jina.
“Gusa kadi mwanzoni na mwisho. Wakati mwingine kutakuwa na kile tunachokiita lango au kizuizi ambapo mnashikilia kadi yenu. Katika hali nyingine, kuna nguzo ya malipo na kisomaji cha kadi,” Prof Nelson anaeleza.

Vipengele vya kawaida vya kadi za kielektroniki ni pamoja na viwango vya upendeleo kwa vijana na wastaafu, nauli za punguzo kwa safari siku za mapumziko na mwishoni mwa wiki, na vile vile viwango vya juu vya bei za kila siku na za kila wiki.
Je, naweza kulipa na kadi ya benki kwa usafiri wa umma nchini Australia?
Kutegemeana na mahali mnaposafiri, mnaweza kulipa kwa pesa taslimu kwa tiketi. Kwa mfano, pesa taslimu bado inakubaliwa huko Western Australia.
Lakini kulipa na kadi ya benki kwa usafiri wa umma kunazidi kuwa jambo la kawaida kote nchini. "Sio majimbo na miji yote ina uwezo huo bado," Howard Collins, Mratibu Mkuu wa Usafiri kwa New South Wales anaeleza.
"Lakini huko NSW kwa mfano, asilimia 60 ya miamala yote sasa ni 'kutumia kadi yenu ya benki'."
“Watu wengi zaidi wanatumia kadi zao za mkopo au debit, wakati mwingine saa zao au simu zao kubonyeza kufika na kuondoka.”
Wakati mnapoangalia kadi ya benki kwenye kisoma kadi kwa ajili ya ukaguzi wa tiketi, afisa wa kufuata sheria anaweza kuona tu taarifa ya malipo yenu, Bwana Collins anaongeza.
“Hivyo, hakuna wasiwasi kuhusu anuani au taarifa nyingine kwenye kadi yenu ya mkopo au debit.”

Maafisa walioidhinishwa wanaweza kuangalia nini katika vituo na ndani ya treni?
Maafisa walioidhinishwa hufanya ukaguzi wa tiketi na usalama, huku kamera za CCTV zikiwa zimewekwa ndani ya treni na kwenye vituo.
Mnashauriwa kuwa na uhakika wa kuwafikia wafanyakazi wa usafiri wa umma kwa masuala ya usalama, Charlotte Hayes anasema.
Yeye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkakati wa Wateja na Mawasiliano katika Mamlaka ya Usafiri wa Umma ya Australia Magharibi.
“Wafanyakazi wetu wa usalama wapo hapa kusaidia. “Hivyo, ikiwa mnaona tabia ya kupotosha au mnakumbana na tabia isiyo ya kawaida mko salama kuzungumza na afisa wa usalama,” Bi Hayes anasema.
Makosa ya usafiri wa umma ni yapi?
Makosa ya usafiri wa umma yanajumuisha makosa yanayohusiana na tiketi na tabia ambazo zinaweza kupelekea kupewa faini au kushtakiwa.
Mfano wa makosa yanayotumika kote Australia ni pamoja na:
- kusafiri bila tiketi halali,
-au bila uthibitisho wa haki yako ya punguzo -
-kuvuta sigara na kunywa pombe -
-kuweka miguu yenu kwenye kiti
Ni nini kinachotokea nikipata faini?
Kama mkiona mmepata faini na mnahisi mmeonewa, mnaweza kutafuta msaada wa kisheria au kupinga faini hiyo kupitia shirika lenu la usafiri wa umma.
"Kuna timu inayoshughulikia ukiukaji. Nendeni kwenye tovuti ya wakala wenu, na mnaweza kupata jinsi ya kukata rufaa dhidi ya ukiukaji huo," Bi Hayes anaeleza.
"Msisahau kuweka faini kwenye droo tu na kusahau juu yake.
Kwa sababu faini hizi zinaweza kuongezeka na […] zinaathiri mkopo wenu, uwezo wenu wa kupata leseni ya udereva na mambo mengine mazito.”
Tabia nzuri ya kutumia usafiri wa umma nchini Australia ni ipi?
Sheria na matarajio ya kawaida wakati wa kutumia usafiri wa umma nchini Australia ni: -
-Kutomsumbua dereva
- Kuwapa nafasi za kukaa wale wanaohitaji
- Kuacha abiria washuke kabla ya kupanda
- Kuepuka kuweka mifuko kwenye viti
- Kuepuka kula chakula chenye harufu kali
Je, ni lazima muwe kimya mnapotumia usafiri wa umma nchini Australia?
Kuweka mazungumzo na muziki kuwa kwa sauti ya chini inatarajiwa kwa abiria kote katika mitandao ya usafiri wa umma ya Australia.
Kumbukeni kwamba kushiriki nafasi hiyo kunamaanisha pia kushiriki sauti na abiria wengine, Bi. Hayes anasema.
"Ni zile tabia njema zinazohakikisha mfumo wa usafiri wa umma unafanyakazi kwa ajili ya kila mtu."
Na daima hakikisheni ikiwa mko kwenye eneo linaloitwa 'kimya', Prof Nelson kutoka Chuo Kikuu cha Sydney anashauri.
Hiyo inamaanisha hakuna mazungumzo kwa sauti kubwa, hakuna kupokea ujumbe wa simu.
“Mabehewa ya utulivu yana heshimika sana, na watu hawapaswi kushangaa ikiwa mgeni kamili anageuka na kusema, 'mnaweza kuacha kuzungumza? Mko kwenye behewa la utulivu.'”
Jisajili au fuateni podcast ya "Australia Explained" kwa maelezo muhimu zaidi na vidokezo kuhusu kuzoea maisha yenu mapya Australia.
Mna maswali au mawazo ya mada? Tutumieni barua pepe kwa australiaexplained@sbs.com.au










