Wachezaji watano wamepewa visa za kibinadamu na Serikali ya Australia asubuhi ya leo Jumanne, baada ya kuchukuliwa chini ya ulinzi wa Polisi wa Shirikisho la Australia.
Takriban watu 700 katika Eneo la Kaskazini wako katika makazi ya dharura kufuatia mafuriko makubwa, huku mji wa Katherine bado ukiwa chini ya onyo la mafuriko ya dharura. Takriban watu 1000 wamehamishwa kutoka eneo hilo katika siku za hivi karibuni. Tahadhari pia zipo kwa sehemu kubwa za Queensland, ikiwa ni pamoja na Brisbane, baada ya kupungua kwa joto ya kitropiki kusababisha mafuriko hatari na kuongezeka kwa kasi kwa kina cha mito.
Nchini kenya idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko yaliosababishwa na mvua kubwa wiki iliopita, imeongezeka kutoka 23 na sasa idadi hiyo imefikia watu 45, kwa mujibu wa taarifa ya polisi nchini humo. Mbali na idadi ya vifo kuongezeka, idara ya polisi nchini humo imesema waru wapatao 2224 pia walilazimika kuyahama makazi yao, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.




