Jimbo la Kusini Australia limefichua mpango wa kwanza wa kupiga marufuku vurugu za majumbani na wahalifu wa kujamiana kutoka kwa programu za kuchumbiana.
Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa
Mwanasheria Mkuu wa jimbo hilo Kyam Maher anasema pendekezo hilo litaboresha usalama kwa wale wanaohusika katika kuchumbiana mtandaoni.
Hatua hiyo inafuatia ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Uhalifu ya Australia mnamo 2022, ambayo iligundua kuwa theluthi moja ya waliohojiwa walifanyiwa ukatili wa kingono na mtu waliyekutana naye kwenye programu au tovuti katika miaka mitano iliyopita.
Bofya hapo juu kwa taarifa zaidi.






