Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Taarifa ya Habari:Vyuo vikuu kukabiliwa na faini kubwa vikishindwa kupambana na ubaguzi wa rangi

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili
Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Serikali ya Shirikisho inasema vyuo vikuu vinaweza kukabiliwa na faini ikiwa vitashindwa kupambana na ubaguzi wa rangi chini ya viwango vipya vilivyoanzishwa Jumatatu 13 Julai 2026.


Published

By Gode Migerano

Presented by Gode Migerano

Source: SBS



Share this with family and friends


Serikali ya Shirikisho inasema vyuo vikuu vinaweza kukabiliwa na faini ikiwa vitashindwa kupambana na ubaguzi wa rangi chini ya viwango vipya vilivyoanzishwa Jumatatu 13 Julai 2026.


Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa

Mabadiliko hayo yanahitaji taasisi za elimu ya juu kupitisha ufafanuzi wa ubaguzi wa rangi, ikiwa ni pamoja na chuki dhidi ya Wayahudi, chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi wa rangi dhidi yawa Aboriginal na wakaazi wa Visiwa vya Torres Strait.

Polisi wa Shirikisho la Australia wamefichua kuwa zaidi ya familia 120 za watoto waliotambuliwa kama waathiriwa wa unyanyasaji na mfanyakazi wa huduma ya watoto wamewasiliana nao.AFP inasema mshtakiwa anayedaiwa ni mwanaume mwenye umri wa miaka 35 ambaye ameshtakiwa kwa makosa zaidi ya 300 yaliyofanywa kwa kipindi cha miaka 16.

Waasi wa AFC/M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wametumia mripuko wa ebola katika eneo wanalolidhibiti kuonyesha uwezo wao wa kuongoza nchi. Wamefanya hivyo kwa kuonyesha uwezo wao wa kuongoza nchi kwa kuanzisha juhudi za kukabiliana na mripuko huo tofauti za zile zinazoendeshwa na serikali ya Kinshasa.

Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now