Mahakama ya Kupambana na Ugaidi na Makosa Dhidi ya Taifa iliyoko mjini Port Sudan nchini Sudan, , imemhukumu kifo kiongozi wa kundi la wanamgambo wa RSF, Mohamed Hamdan Daglo pamoja na maafisa wengine 15 wa RSF.
Idara, ya Mambo ya Nje na Biashara inafanya uchunguzi wa haraka na mamlaka za mitaa ili kubaini kama kuna Waaustralia wowote walioathiriwa na moto mbaya huko Bangkok. Angalau watu 27 wamefariki - na wengine 63 wamejeruhiwa - baada ya moto kuzuka kaskazini mwa mji mkuu wa Thailand [[Jumatatu]].
Wazima moto walichukua takriban nusu saa kudhibiti moto huo, huku chanzo cha moto huo kikichunguzwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Telstra atafika mbele ya uchunguzi wa Seneti kujibu maswali kuhusu mfumo wa dharura wa Australia Ijumaa hii [[17 Julai]], baada ya kupotea kwa huduma za kampuni hiyo kote nchini kusababisha machafuko wiki iliyopita.
Kamishna huru wa kwanza wa Waathiriwa wa Uhalifu jimboni New South Wales anasema atatumia nafasi hiyo kuhakikisha waathiriwa-wahanga wanasikilizwa katika ngazi za juu za serikali.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






