Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Taarifa ya Habari:Polisi wachunguza kama kifo katika jimbo la Kusini Australia, kina husishwa na kupotea kwa huduma za Telstra Jumatano

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili
Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Polisi wanachunguza kama kifo kinahusishwa na kupotezwa kwa huduma ya Telstra kote nchini Jumatano. Wapelelezi wa Kusini Australia wamethibitisha mtu mmoja alifariki katika hospitali ya kanda Jumatano, lakini polisi hawakuwa wamearifiwa kuhusu kifo hicho.


Published

By Gode Migerano

Presented by Gode Migerano

Source: SBS



Share this with family and friends


Polisi wanachunguza kama kifo kinahusishwa na kupotezwa kwa huduma ya Telstra kote nchini Jumatano. Wapelelezi wa Kusini Australia wamethibitisha mtu mmoja alifariki katika hospitali ya kanda Jumatano, lakini polisi hawakuwa wamearifiwa kuhusu kifo hicho.


Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa

Afisa wa polisi wa New South Wales amekamatwa baada ya kupatikana na hatia ya kumkaba koo na kumnyanyasa kingono mkewe wa wakati huo.Jaji alifuta dhamana ya afisa huyo kabla ya hukumu yake mwezi Novemba, akielezea kosa hilo kuwa kubwa sana.

Afisa huyo, ambaye hawezi kutambuliwa ili kulinda utambulisho wa mwathiriwa, alihukumiwa kwa makosa 11 yanayohusiana na unyanyasaji wa nyumbani, ikiwa ni pamoja na ngono bila ridhaa na shambulio linalosababisha madhara halisi ya mwili.

Maridhiano mapya ya kisiasa kati ya vyama vikuu vya Zanzibar, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo, yamefikiwa rasmi leo baada ya viongozi wa pande hizo mbili kusaini tamko la pamoja. Amko hilo limesomwa Ikulu Zanzibar na Katibu Mkuu Kiongozi, Mansura Mossi Kassim, mbele ya viongozi wa serikali, viongozi wa dini na wawakilishi wa vyama vya siasa. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aliyeshuhudia utiaji saini huo.

Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now