Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Mbappé aiweka Ufaransa katika nusu fainali

(SP)U.S.-BOSTON-FOOTBALL-FIFA WORLD CUP-QUARTER FINAL-FRA VS MAR
Kylian Mbappe of France celebrates scoring during the quarter final match between France and Morocco at the 2026 FIFA World Cup in Boston. Photo by Xinhua/Sipa USA. Source: SIPA USA / Lui Siu Wai/Xinhua/Sipa USA

Ufaransa imetinga nusu fainali ya Kombe la Dunia, baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Morocco. Kylian Mbappé amefunga mabao nane sawa na Lionel Messi, wakati Ousmane Dembélé akikamilisha ushindi huo.


Published

Updated

By Gonzalo Aguirregomezcorta

Presented by Gode Migerano

Source: SBS



Share this with family and friends


Ufaransa imetinga nusu fainali ya Kombe la Dunia, baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Morocco. Kylian Mbappé amefunga mabao nane sawa na Lionel Messi, wakati Ousmane Dembélé akikamilisha ushindi huo.


Mbappé aling’aa Ufaransa ilipoishinda Morocco 2-0 mjini Boston na kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia ya tatu mfululizo. Ufaransa uli funga magoli mawili katika muda wa dakika sita, Mbappe akifunga goli la kwanza katika dakika ya 60, kabla ya Dembélé kufunga bao la pili nala ushindi muda mfupi baadae.

Kesho Jumamosi, Uhispania ambayo inapigiwa upatu katika mashindano hayo, itakabiliana na nyota wa Ubelgiji mjini Los Angeles. Kufikia sasa Uhispania haija ruhusu goli lolote katika Kombe la Dunia na sasa, watakabiliana na Wabelgiji ambao wamefunga magoli 12 katika mechi 3 zilizo pita, ikijumuisha mechi waliyotoka nyuma dhidi ya Senegal pamoja na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya wenyeji wenza Marekani.

Jumapili, pambano la ulaya lita endelea kupitia Norway dhidi ya Uingereza, na baadae Argentina itapambana na Uswisi.

Tazama kila dakika ya Kombe la Dunia la FIFA 2026™ mubashara na bila malipo kwenye runinga ya SBS na mtandaoni kupitia SBS OnDemand.

Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now