Nusu fainali za Kombe la Dunia zimewadia, Ufaransa na Uhispania zikijiandaa kufufua moja ya ushindani mkubwa wa soka la kimataifa. Tunaangalia kwa karibu habari za hivi punde za timu hizo na kusikia kutoka kwa kambi zote mbili kabla ya pambano kubwa la kesho.
Sikiliza makala yetu yaliyo rekodiwa hapa
Ni moja ya mechi zinazotazamiwa sana za mashindano hayo. Ufaransa na Uhispania zitakutana mjini Dallas kesho zikiwania nafasi katika fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026. Kwa Ufaransa, mechi hiyo ina umuhimu wa ziada, huku nusu fainali ikiangukia katika siku ya Bastille, mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia kuwahi kuchezwa katika siku ya kitaifa ya nchi hiyo.
Uhispania imekuwa mojawapo ya timu zilizokamilika zaidi katika mashindano haya, ikichanganya soka la kumiliki mpira linalotawala na ulinzi imara ambao umeruhusu goli moja tu katika mbio zake za kufika katika nusu fainali.
Alhamisi, Argentina itacheza dhidi ya Uingereza katika nusu fainali ya pili yakusisimua. Matangazo ya moja kwa moja pia yakianza saa 10 usiku, kwa masaa ya mashariki ya Australia.
Tazama kila dakika ya Kombe la Dunia la FIFA 2026™ moja kwa moja na bila malipo, kwenye runinga ya SBS na mtandaoni kupitia SBS OnDemand.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






