Taarifa zimeibuka kuwa Katherine Deves alitoa madai mtandaoni yakibaguzi dhidi ya watu wenye jinsia tofauti, kauli ambayo ameombea msamaha. Wakati huo huo upinzani ume apa kuanzisha tume ya uchunguzi wa ufisadi wa shirikisho kufikia mwisho wa mwaka huu ukishinda uchaguzi mkuu.
Tukisalia katika maswala ya kampeni, mbunge wa chama cha Labor Chris Bowen alikuwa anatarajiwa kujiunga na kampeni ya Bw Albanese jimboni Queensland ila, amelazimishwa kuingia katika karantini baada ya vipimo vyake vya UVIKO-19 kurejesha matokeo chanya. Bw Bowen ni mbunge wa tatu aliye ambukizwa wiki hii, baada ya msemaji wa maswala ya nyumbani katika chama cha Labor Kristina Keneally na Waziri wa maswala ya nyumbani Karen Andrews.
Kampeni hizo zilisitishwa kwa sababu ya Pasaka ya Jumapili.