Ameongezea kuwa lazima pawe gharama kwa matendo ya Moscow, akidokeza kuwa huenda vikwazo vya ziada vita tangazwa.
Australia imeweka vikwazo vya marufuku ya safari pamoja na adhabu yakifedha, kwa wanachama wanane wa baraza la kitaifa la ulinzi ya Urusi na, kulenga sekta maalum zinazo taka kujitenga katika kanda ya Ukraine kama Donetsk na Luhansk, pamoja na benki sita za Urusi.
Hata hivyo Ubalozi wa Urusi mjini Canberra umeishtumu serikali ya Australia kwa "kuunga mkono nakuhimiza wachocheaji wa chuki dhidi ya wageni ambao wako Kyiv" na kuwa "uamuzi wakutambua miji ya Donetsk na Luhansk ulifanywa kwa misingi yakibinadam, nakuwalinda raia." Naye Bw Morrison alijibu shtuma hizo kwa kusema kuwa, kuwatambua wanajeshi wa urusi kama walinda amani ni matusi kwa sababu: