Uvumbuzi uliofanywa na wanasayansi hao, umekuja muda muafaka wakati ni takribani vifo mia tatu kutokana na virusi hivyo vimetangazwa kutokea mwaka huu ikiwa vimeanza mapema isivyotarajiwa katika msimu wa mafua.
Jimbo la Kusini Australia lime pata pigo kubwa zaidi. Idadi ya watu 82 wengi wao wakiwa wazee, wame fariki katika jimbo hilo mwaka huu, na idadi kamili ya visa vya mafua inakaribia elfu 20. Kulinganisha na wakati kama huo mwaka jana, kulikuwa na visa elfu 1500 ambavyo vilikuwa vimethibitishwa.
Hali hiyo imesababisha upinzani kutoa wito wa tathmini, ya jinsi serikali inashughulikia msimu wa mafua, pamoja na uwepo wa vifaa vyakutosha vya chanjo.