Les alikuwa mmoja wa watu walio kuza kandanda nchini Australia, akishirikiana na rafiki yake wa karibu ambaye pia alikuwa mchezaji wa zamani wa Australia Johnny Warren.

Hatakama rafiki yake haku fanikiwa kushuhudia Australia ikikabiliana na vigogo wa soka katika kombe la dunia baada ya miaka mingi ndani ya jangwa la soka, Les Murray aliongoza matangazo ya soka kwa ufanisi ndani ya nyumba zawa Australia kila siku.

Les aliongoza matangazo ya soka kwa mara ya mwisho katika michuano ya kombe la dunia ya FIFA nchini Brazil mwaka wa 2014. Aliwaaga watazamaji kwa mara ya mwisho akizungukwa na marafiki na washiriki, pamoja naku acha urithi utakao wa faidi waandishi wa habari kwa miaka mingi ijayo.

Hata kama jamii ya kandanda ya Australia imempoteza mwanao mpendwa, hakuna shaka urithi wake uta ishi nakudumu milele.
Share
