Rahab Joy Sinclair ni kiongozi wamabalozi wa maswala ya afya ya akili jimboni New South Wales, katika shirika la Mental Health Foundation Australia. Bi Rahab atakuwa mmoja wa wazungumzaji katika sherehe ya uzinduzi wa mwezi wa afya ya akili. Mandhari ya mwezi wakitaifa wa afya ya akili ni: Changamoto za uponaji baada ya janga na uthabiti
Katika mazungumzo maalum, Bi Rahab ali eleza idhaa ya Kiswahili ya SBS umuhimu, wajamii zenye asili ya Afrika kushiriki katika matukio mbali mbali yanayo andaliwa katika mwezi wa afya ya akili.
Bi Rahab atachangia hadithi yake kuhusu changamoto za afya ya akili, zilizo mkabili na jinsi alivyo zimudu. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu jinsi unaweza shiriki katika matukio ya mwezi wa afya ya akili, pamoja na mahojiano ya Bi Rahab: www.mhfa.org.au/CMS/about-mhfa