Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE starting June 12 2026

Makala leo: 'Punguza uchochezi' Waziri Mkuu asema baada ya ongezeko ya vitisho dhidi ya wabunge

The Prime Minister’s residence The Lodge is seen in Canberra.

The Prime Minister’s residence The Lodge is seen in Canberra, Wednesday, February 25, 2026. (AAP Image/Mick Tsikas) NO ARCHIVING Source: AAP / MICK TSIKAS/AAPIMAGE

Kuondolewa kwa dharura kwa Waziri Mkuu kutoka nyumbani kwake mjini Canberra kwa sababu ya tisho la bomu lililolengwa, kumesababisha maonyo ya kuongezeka kwa mazingira ya usalama, ambapo uadui mtandaoni unazidi kujitokeza kama vitisho vya kimwili vyenye madhara makubwa.


Published

By Briana Charles

Presented by Gode Migerano

Source: SBS



Share this with family and friends


Kuondolewa kwa dharura kwa Waziri Mkuu kutoka nyumbani kwake mjini Canberra kwa sababu ya tisho la bomu lililolengwa, kumesababisha maonyo ya kuongezeka kwa mazingira ya usalama, ambapo uadui mtandaoni unazidi kujitokeza kama vitisho vya kimwili vyenye madhara makubwa.


Hali hii inafuatia maoni ya Kamishna wa Polisi wa Shirikisho mwishoni mwa mwaka jana, akibainisha mwenendo wa kuongezeka kwa vurugu dhidi ya maafisa wa umma.

Kufuatia tisho la bomu lililotolewa kwa lugha ya Mandarin dhidi yake na maafisa wengine wakuu, Waziri Mkuu Anthony Albanese alihamishwa kwa masaa kadhaa kutoka makazi yake ya Canberra siku ya Jumanne.

Madai ya uongo yalitolewa kwamba vilipuzi vilikuwa vimetegwa ili kulipua makazi ya Waziri Mkuu kuwa magofu, siku chache kabla ya onyesho lililopangwa kufanywa na kundi la Shen Yun Performing Arts.

Kampuni hiyo ya densi yenye makao yake makuu mjini New York imekuwa ikikosoa chama cha kikomunisti cha China, na imepigwa marufuku nchini China. Kampuni hiyo inakabiliwa na shinikizo na madai yanayoendelea ya kufuta maonyesho yake ya kimataifa.

Bonyeza hapo juu kwa makala kamili.


Latest podcast episodes

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now