Utafiti mkubwa zaidi nchini Australia kuhusu mazingira ya kazi ya wahamiaji umefichua maelezo ya kutisha ya malipo duni yaliyoenea na ya kimfumo.
Utafiti huo, uliochapishwa na asasi ya Migrant Justice Initiative, unaonyesha kuwa theluthi mbili ya wafanyakazi wahamiaji wanalipwa kiasi kidogo kuliko kile wanachostahili kisheria, chini ya Sheria ya Kazi ya Haki, na wanafunzi wa kimataifa pekee wanadhulumiwa dola bilioni 3.18 za mishahara kila mwaka.
Waandishi wa ripoti hiyo wanasema kuwa utafiti huo pia unatoa maarifa mapya muhimu kuhusu jinsi waajiri wanavyoficha unyanyasaji huo.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.






