Mfumo wa utoaji wa mayai ya uzazi Australia huenda ukabadilika

A composite image of a needle entering an egg under a microscope and the shadow of three children

Source: SBS / Karin Zhou-Zheng

Mahitaji ya mayai ya uzazi yanaongezeka nchini Australia kadiri watu wanavyokumbwa na changamoto za uzazi. Lakini mahitaji ya mayai ni makubwa mno kuliko upatikanaji wao na sasa, wataalamu wanapendekeza Australia ifikirie kubadilisha kanuni zinazohusu utoaji mayai.


Liz Buckley Stokes anasema kwamba amekuwa akitamani kuwa mama , lakini imechukuwa muda asiotarajia .

Mimi na mume wangu tulifunga ndoa tukiwa na umri mkubwa kidogo, hivyo tulitamani sana kupata Watoto, na njia pekee tuliyoweza kutumia ilikuwa kupitia utoaji wa mayai. Nilikuwa na umri wa miaka arobaini na saba 47, hivyo umri wangu ulikuwa kwa kiasi kikubwa
Liz Buckley Stokes

Liz, ambaye sasa yuko kwenye umri wa miaka 50 na anaishi katika Pwani ya Sunshine, anasema alijiunga na majukwaa ya mtandaoni ya uchangiaji wa mayai, lakini ilichukua takriban miezi saba kupata mdhamini.

 
Ni mchakato mrefu sana na unaochosha , na ni mgumu kweli kwa kuwa mnajitokeza pale na hampati kitu, na ni kitu kinachokatisha tamaa sana , wakati mnawaza kwamba hutapata kuwa mama na hampati nafasi hiyo kwa sababu hakuna anayejibu tangazo lenu
Liz
 

Liz amekuwa na watoto watatu tangu wakati huo akitumia mayai kutoka kwa mfadhili yule yule: mvulana wa miaka sita na mapacha wawili wa miaka minne. Pia anasema amedumisha uhusiano wa karibu na mfadhili aliyewawezesha.

 

 
Sababu zake za kuwa mfadhili zilikuwa kwamba yeye mwenyewe alipitia utaratibu wa IVF kwa sababu alilazimika kuondolewa mirija yake ya uzazi, hivyo alielewa mchakato huo na alielewa uchungu unaohusiana na hali hiyo.
Liz

Ingawa mchakato huo ulidumu kwa muda, Liz anajiona kuwa na bahati kupata mtoaji wa mayai kabisa.
Tangu watoto wa kwanza wa I-V-F walipozaliwa mwanzoni mwa miaka ya elfu moja mia tisa themanini sekta ya uzazi imekua kwa kasi na sasa karibu mtoto mmoja kati ya kumi na sita anayezaliwa Australia hupatikana kupitia I-V-F, huku mahitaji ya mayai yaliyotolewa yakiwa mengi zaidi kuliko usambazaji wake nchini Australia.

Mtafiti mwandamizi katika Shule ya Afya ya Umma ya Chuo Kikuu cha Monash, Daktari Karin Hammarberg, anasema ongezeko la changamoto za uzazi linaendesha mahitaji ya mayai yaliyotolewa.

Kwa ujumla kama jamii, wanawake wengi wanapata watoto wakiwa na umri mkubwa au wanaanza kufikiria kupata mtoto wakiwa na umri mkubwa kuliko zamani. idadi ya wanawake wanaojaribu kupata watoto wakiwa na miaka ya mwisho ya thelathini au mwanzo wa arubaini ni kubwa zaidi sasa kuliko ilivyokuwa miaka ishirini iliyopita, na hilo linamaanisha wale wanaokaribia miaka ya arubaini 40 au walio na miaka arobaini. Wengi wao wanapata changamoto ya kuweza kushika mimba.
Karin Hammerberg
Dkt. Hammarberg anasema kwamba mara nyingi wanawake hawa wanaelekezwa kutumia mayai yaliyotolewa na wachangiaji.

Wanaweza kuyapata kwa njia mbili nchini Australia: kupitia uhusiano wa kibinafsi kama Liz au kupitia kliniki za IVF. Hata hivyo, Daktari anasema utoaji bado ni nadra.


[Hapa Australia, mara nyingi utoaji wa mayai hufanyika kupitia uhusiano unaojulikana. Hivyo basi, mtu anakuja kliniki akiwa na dada, binamu au mtu mwingine wa familia ambaye yupo tayari kufanya hivyo kwa ajili ya mtu huyu mahsusi , lakini hayupo tayari kufanya hivyo kwa yeyote yule. Na hapo ndipo shida ilipo. Hatuna watu wa kutosha walio tayari kufanya mambo haya yote bila manufaa yoyote ya kibinafsi.
Dkt. Hammerberg

Ingawa idadi halisi ya watu wanaosubiri mayai yaliyotolewa haijulikani, utafiti mmoja kutoka Chuo Kikuu cha Melbourne uligundua kuwa kati ya wanawake Hamsini na tisa waliowekwa kwenye orodha ya kusubiri mchango wa mayai katika kliniki ya IVF, ni kumi na tatu tu waliopewa yai la mtoaji.

Stephen Page ni wakili wa masuala ya uzazi kutoka kampuni ya sheria ya familia ya Page Provan. Anasema mahitaji haya yamewasababisha watu kutumia mayai yaliyoagizwa kutoka nje ya nchi. 
[atika miaka michache iliyopita, kumekuwa na uingizaji wa mayai kutoka nje kuingia Australia. Sasa, tunaona mayai yakiwa yameingizwa kutoka Marekani, Malaysia na Ukraine, pamoja na nchi nyinginezo
Stephen Page
 
Baadhi ya wazazi wenye matumaini pia husafiri kimataifa kununua mayai na kufanyiwa matibabu ya uzazi - ingawa nchi nyingine zinaweza kuwa na viwango tofauti vya sheria na maadili kwa mchakato huo.

 Nchini Marekani, kwa mfano, wachangiaji wanaweza kulipwa pesa kiasi kikubwa kwa mayai. Lakini huku Australia, vyovyote vile vishawishi vya kifedha vya moja kwa moja au visivyo vya moja kwa moja ni kinyume cha sheria - ambayo Daktari Hammarberg anasema kuwa ni hali ya kushangaza kabisa.


Katika mazingira ambapo kila mtu analipwa, daktari analipwa, kliniki inalipwa, mpokeaji analipa pesa nyingi, mtu pekee asiyepokea fidia yoyote ni mwanamke anayefanya kazi halisi. Hilo haliendani na ufahamu wetu wa kile kinachowiana.
Stephen Page
Ili kujaribu kushughulikia uhaba wa mayai, wataalamu sasa wanahoji kuwa Australia inaweza kubadilisha mbinu yake ya utoaji wa yai.

Uingereza, wanawake hawalipwi kwa utoaji wa yai, lakini wafadhili wanaweza kupokea malipo ya karibu dola elfu mbili kwa kila mzunguko kuwalipia gharama zao.

Wanawake pia wanaweza kudai malipo ya ziada kwa gharama kama vile kusafiri, malazi, na malezi ya watoto. Daktari Hammarberg ametaja kuwa inaweza kuwepo malipo yaliyowekwa hapa Australia pia.

 
Kwa namna fulani, ninafikiri lazima kuwe na njia ya kati ambapo kuna aina fulani ya kutambua jitihada na kuthamini ukweli kwamba mwanamke anachukua hatari na anapitia haya yote
Dkt. Hammerberg

 

Stephen Page anakubali kwamba Australia inaweza kufanya mabadiliko kadhaa na anapendekeza kuwa wanawake wanaweza kupewa taarifa bora kuhusu uwezekano wa mayai waliyohifadhi tayari katika kliniki za IVF kwa matumizi binafsi.

Inakadiriwa kuwa kuna takriban mayai laki moja yanayohifadhiwa kwa sasa nchini Australia. Na utafiti mmoja uliochunguza miaka kumi ya uhifadhi wa mayai huko Victoria, uligundua kuwa chini ya asilimia 13 ya wagonjwa walirudi kutumia mayai yao kila mwaka.

Tuna mayai mengi sana yanayohifadhiwa lakini ni machache tu kati ya hayo yanatolewa au kutumiwa. Sehemu ya tatizo ni kwamba tunayo mayai haya yote kwenye hifadhi, hakuna au ni machache yanayotolewa kwa ajili ya michango na labda hayatatolewa, lakini kama baadhi ya wanawake hao watatiwa we moyo na kushauriwa na wako tayari kutoa, itasaidia kutatua tatizo hili.
Stephen Page
Bwana Page anasema kwamba hatimaye, kutumia mayai kutoka kwa wafadhili wa ndani kunaweza kufanya haki zaidi kwa watoto waliozaliwa kutokana na ujauzito huo]].

Tukiangalia mtazamo wa mtoto, watu wengi waliosanifiwa kwa msaada wa mchango wanataka kujua walipotoka. Ikiwa wanajua kwamba mtoaji yuko mahali fulani Australia, inafanya kuwa rahisi zaidi. Ni rahisi na rahisi zaidi. Wako chini ya barabara au katika jimbo jingine, hawako upande mwingine wa dunia ambapo huwenda sitawapata.
Stephen Page
Hata hivyo, ni vigumu mabadiliko haya kutokea hivi karibuni, na wakati suala la ugavi na mahitaji la Australia linasalia, Liz anasema atajaribu kuunganisha wafadhili na wazazi wanaotumaini kupitia kundi lililoko mtandao wa Facebook, ambalo sasa analisimamia. Anasema anaona athari zinazoendelea za ukosefu wa mayai ya wafadhili kila siku.

Ninawajua wanawake kadhaa kwenye kundi ambao nimezungumza nao binafsi na kuwapelekea ujumbe kwenye Facebook na bado hawajapata mfadhili. Mmoja wao amekuwa kwenye kundi karibu tangu kilipoanza, kwa hivyo ni kama miaka mitano sasa. Ni vigumu sana na inavunja moyo wangu ninaposikia hadithi zao. Hakuna mengi zaidi ninayoweza kufanya kuliko kuwapa msaada na jukwaa.
Liz Buckley Stokes


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service