Shirika kubwa zaidi huru la habari nchini Uganda Nation media group limearifu kuwa limewekwa chini ya ulinzi mkali wa kijeshi mapema Jumapili.
Hatua hiyo inafuatia amri iliyotolewa na Mkuu wa jeshi, Jenerali Muhoozi Kainerugaba aliyeamuru kufungwa kwa televisheni, redio na magazeti ya chombo hicho. Mkuu huyo wa jeshi la Uganda ameeleza wazi kuwa haamini katika uhuru wa vyombo vya habari na kwamba vyombo hivyo vinapaswa kufuata maagizo ya serikali.
Duru ya tatu ya vikao kama sehemu ya Tume ya Kifalme kwa Chuki dhidi ya Wayahudi na Mshikamano wakijamii imeanza.Lengo la wiki mbili zijazo niku chunguza jinsi chuki dhidi ya wayahudi husambaa katika jamii za mtandaoni, madhara yake kwa jamii ya Wayahudi na, ufanisi wa sera zilizopo za kuzuia kauli za chuki.
Bofya hapo juu kwa taarifa zaidi.






