MZIO WA KARANGA KWA WATOTO UPATA MWELEKEO MPYA

Miaka kumi baada ya utafiti muhimu kudhibitisha kwamba kuwalisha watoto wachanga bidhaa za karanga inaweza kuendeleza mzio hatari, utafiti mpya umebaini kuwa kuna uwezekano wa kuepuka kuendeleza mizio ya chakula.


 

Tiffany Leon ni mtaalamu wa lishe kutoka Maryland, Marekani - na pia mama wa wavulana wawili. Walipokuwa wadogo, alifuata mwongozo mpya - uliotolewa kwanza Marekani mwaka 2015 - wa kuwajulisha karanga mapema.

Kama mtaalam wa lishe, natumia mapendekezo yanayotokana na ushahidi katika kazi yangu yote, na hivyo mtu aliponiambia, 'Ah hivi ndivyo sasa inavyofanyika, hizi ni miongozo mipya', nilifikiria tu, 'Ah sawa, basi hivi ndivyo tutakavyofanya'... Kwa hivyo, takriban miezi minne, hadi mitano sisi tulimweka kwenye kiti na kumlisha vyakula vyenye uwezekano mdogo wa kusababisha mzio. Nafikiri tulianza na maharage ya kijani, chakula cha nafaka kwa watoto wachanga, unajua, tulianza na vitu vichache kwanza.
Tiffany Leon

 

Sababu ya mabadiliko haya katika familia ya Leon ni kwa sababu hadi kufikia wakati huo, wazazi waliambiwa kuepuka kuwapea Watoto wao vyakula ambavyo vinaweza kuwa na hatari hadi watakapofikisha miaka mitatu, kwa matumaini ya kuepuka mzio uliokithiri. Mzio wa karanga ni mojawapo ya hali hizi za kawaida, unaosababishwa na pale mfumo wa kinga wa mwili unapokosea na kutambua protini katika karanga kama hatari na kuachilia kemikali zinazozua dalili kama vile vipele, matatizo ya upumuaji, na wakati mwingine, anaphylaxis inayoweza kuhatarisha maisha. Katika tukio hilo, kama vile mzazi huyu alivyoiambia SBS mnamo Agosti, inaweza kuwa hali inayochukua kila kitu.

Mizio si kero tu. Kwa kweli, zinaathiri kila kipengele cha maisha ya familia
Tiffany Leon

 

Mwongozo mpya unaolenga kuepuka matokeo ya aina hii ulitolewa katika nchi kadhaa baada ya Gideon Lack kutoka Chuo cha King London kuchapisha utafiti wa kihistoria wa Learnin Early About Peanut allergy ama LEAP, kazi ambayo ilidokeza kwamba kufichua mapema kunaweza kusaidia watoto. Daktari David Hill, kutoka Hospitali ya Watoto ya Philadelphia anaeleza zaidi.
Utafiti wa LEAP... ulionyesha kwamba ikiwa tutawatambulisha watoto kwa mizio hiyo kupitia mdomo, kwa kuwa na wao kuila, kabla ya kuwasiliana nayo kupitia ngozi yao, tunaweza kupunguza hatari ya mtoto huyo kuendelea kupata mzio wa chakula
Dkt.Hill
 

 

Watoto wa Virginia wanaonekana kuepuka kupata mzio wa karanga - na sasa Daktari Hill ameweza kuchapisha utafiti mpya baada ya kuchambua rekodi za afya za kielektroniki kutoka kwa madaktari wa watoto ili kufuatilia utambuzi wa mizio ya chakula kwa watoto wadogo kabla, wakati na baada ya miongozo mipya kutolewa. Imepatikana kwamba maelfu ya watoto wengine nchini Marekani pia wameepuka kupata mzio wa karanga baada ya wazazi wao kufuata ushauri sawa wa lishe kama ule wa kina Leon.
Kile ambacho data yetu inaonyesha ni kwamba kutokana na, au angalau kwa kuhusiana na miongozo ile ya utambulisho wa mapema, kuna takriban watoto elfu sitini 60,000 wachache wanaosumbuliwa na mzio wa vyakula leo kuliko ambavyo ingekuwa. Na hiyo ni jambo la kushangaza, sivyo? Hiyo ni saizi ya baadhi ya miji
Dkt.Hill

 

Rachel Peters, Profesa Mshiriki, ni Kiongozi wa Mpango wa Utafiti wa Afya ya Idadi ya Watu katika Kituo cha Kitaifa cha Ubora wa Mzio cha Taasisi ya Utafiti ya Watoto ya Murdoch. Amekuwa sehemu ya utafiti katika Taasisi hiyo ambao pia unachunguza masuala haya. Kulingana na kundi la kujitolea la Allergy na Anaphylaxis Australia, mzio wa karanga ni mojawapo ya mizio ya chakula inayotokea zaidi utotoni nchini Australia, ikiathiri asilimia 3 ya watoto wachanga hadi umri wa miezi 12.

 

 

Daktari Peters anasema angalau tafiti mbili kubwa zilikamilika nchini Australia katika muongo uliopita kuchunguza ni nini kinaweza kuzuia mzio huo tangu mwanzo - utafiti mmoja ulifanyika kabla Australia kupitisha miongozo mipya ya lishe ya watoto wachanga mwaka 2016, na mwingine baada ya tarehe hiyo.
Tulikuwa na tafiti mbili za kizazi zilizofanyika katika kanda ile ile, ambayo ilikuwa Melbourne, Australia... Kwa hivyo tulikuwa na makundi mawili yaliyokusanywa kwa mbinu sawa kabisa, lakini baada ya miaka 10 tofauti... Kwanza, tulipima kile wazazi walikuwa wakifanya katika suala la mazoea ya kulisha watoto wachanga na tulikuwa na matokeo ya kuahidi sana yanayoonyesha kuwa karibu asilimia 90 ya watoto wachanga leo wanapewa karanga katika mwaka wa kwanza wa maisha, na hili ndilo ambalo miongozo inashauri kwa sasa... na pili, tulionyesha kwa hakika kushuka kidogo kwa mzio wa chakula, lakini labda sio kama tulivyokuwa tukitarajia
Dkt.Peters
 

Dkt. Peters anasema kuwa matokeo ya Australia yanadokeza kuwa utafiti zaidi unahitajika kufanywa ili kubaini sababu mbalimbali za mzio wa chakula.
 
Ingawa kwa hakika tunaona kupungua kwa viwango vya mzio wa karanga huko Australia, bado viwango viko juu zaidi - na juu zaidi kuliko katika baadhi ya nchi nyingine duniani, na juu zaidi kuliko ilivyoonyeshwa katika utafiti huu wa Amerika pia
Dkt.Peters

 

 Profesa Peters anasema baadhi ya utafiti huo umeonyesha ushahidi wa kutia matumaini.

 



 

Kwa mfano, kuna jaribio kubwa linaloendelea kuchunguza kama kuongeza Vitamini D kwa watoto katika mwaka wa kwanza wa maisha kunasaidia kuzuia mzio wa chakula. Kuna tafiti kadhaa zinazoonyesha kwamba watoto wanaoishi mbali zaidi na ikweta - hivyo wanapata mwanga wa jua kidogo na Vitamini D kidogo - wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata mzio wa chakula. Tunashuhudia hata hilo ndani ya Australia. Tuna viwango vya juu vya mzio wa chakula huko Melbourne ikilinganishwa na tunavyoshuhudia huko Queensland.
Professor Peters

nchini Marekani, Dkt Hill ametiwa moyo na matokeo yake.
Ni jambo la ajabu kwangu kuweza kukaa hapa pamoja nanyi leo na kusema, kwa mara ya kwanza katika historia ya kisasa, siyo tu kwamba tumeweza kupunguza kiwango cha utambuzi wa aleji za chakula, lakini pia tupo chini zaidi kuliko tulivyokuwa miaka mitano iliyopita
Dkt.Hill
 

Wakati huo huo, Dkt. Peters anasema wazazi wanaweza kutuliza akili zao.

 

Wazazi wanapaswa kusikia vizuri na kuwa na uhakika kuhusu aina hii ya utafiti. Wazazi wanapaswa kuwa na imani na wanachofanya leo kulingana na mapendekezo ya ((kulisha watoto wachanga
Dkt Peters
 

 



Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service