Mexico ime ingia katika hatua ya mchujo, baada ya kuishinda Jamhuri ya Korea katika siku ambayo iliadhimishwa na jeraha kubwa nchini Canada.
Katika kundi hilo hilo, Afrika Kusini iliweka ndoto zao za Kombe la Dunia hai, ikipata sare ya 1-1 dhidi ya Czechia kupitia penati katika dakika ya themanini.
Hapo awali, Canada ili icharaza Qatar 6-0 mjini Vancouver, huo ulikuwa ushindi wa kwanza wa taifa hilo katika Kombe la Dunia na ushindi mkubwa zaidi wa timu yoyote kutoka Amerika ya Kaskazini na visiwa vya Karibean katika historia ya Kombe la Dunia la wanaume.
Kuhesabu kumeanza, na hesabu iko wazi: ushindi wa Socceroos dhidi ya mwenyeji Marekani uta hakikisha nafasi yao katika hatua ya mchujo. Wachezaji wote wa Australia wako tayari kuchaguliwa kwa mechi hiyo na Kocha Tony Popovic, kwa ajili ya mechi dhidi ya Marekani Jumamosi tarehe 20 Juni.
Tazama kila dakika ya Kombe la Dunia la FIFA 2026™ katika runinga ya SBS na kupitia SBS On Demand.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.






