Majukwaa makuu manane ya mitandao ya kijamii yatakuwa chini ya marufuku kali ya mitandao ya kijamii kwa walio chini ya umri wa miaka 16 nchini Australia.
Kuanzia tarehe 10 Desemba, watumiaji walio chini ya miaka 16 watazuiwa kufikia Reddit, Kick, Facebook, Instagram, Snapchat, TikTok, YouTube, na X, majukwaa ambayo Waziri wa Mawasiliano Anika Wells anasema yalitambuliwa baada ya tathmini na Kamishna wa Usalama wa Mtandaoni.
Wakati baadhi ya wakosoaji wanasema kwamba orodha hiyo imekuja kuchelewa, Waziri Wells anasema ni kazi inayoendelea ya Kamishna kutathmini kampuni kulingana na mahitaji ya kisheria.
Tathmini za majukwaa ya usalama wa mtandao zitakuwa endelevu na itaendana na mabadiliko ya kiteknolojia, lakini tunaelewa kuwa familia zinahitaji uhakika sasa kuhusu majukwaa makuu yaliyo chini ya sheria za umri wa chini kwenye mitandao ya kijamii.Anika Wells
Reddit na jukwaa la Kick, ndio nyongeza za hivi karibuni kwenye orodha ya majukwaa. Kamishna wa eSafety, Julie Inman Grant, anasema ushirikiano huu unatokana na jinsi sheria inavyotofautisha kati ya michezo ya mtandaoni na ujumbe wa kijamii.
Jambo lingine la kuzingatia kwetu ni ikiwa jukwaa linakidhi vigezo vya darasa la huduma ambapo kuna upendeleo, kama vile ujumbe, michezo mtandaoni au maudhui ya elimu. Teknolojia inabadilika kwa kasi na daima inakua, ambayo ina maana kwamba orodha hii itabadilikaJulie Grant
Bi. Grant amesisitiza tofauti hii alipohojiwa kwanini majukwaa kama twitch au steam hayakujumuishwa
Tulipima jukwaa la Steam na mazungumzo ya Steam kando... Tulitathmini kwamba Steam ina madhumuni manne ya sasa... Yaliangukia zaidi katika jukwaa la michezo ya mtandaoni, na yaliangukia ndani ya kundi la huduma zilizoorodheshwa kwenye sheria kama zilitengwa kwa sababu madhumuni yao makuu ni kuwawezesha watumiaji kucheza michezo ya mtandaoni na watumiaji wengine, ingawa bado kuna mwingiliano wa kijamii wa mtandaoni kama sehemu ya vipengele vyao. Kwa hivyo Twitch bado inaendelea kutathminiwa.Bi.Grant
Jambo linaloshtua kote duniani ambapo wasichana wa Australia wanamulengwa na wanaume wenye nia mbaya, linafanyika kwenye majukwaa kama Roblox.
Bi Grant ameulizwa kwanini basi Roblox haikuingizwa kwenye sheria hata kama kitaalam ilikuwa jukwaa la michezo ya mtandaoni. Waziri Wells na Bi Grant wamesema kuwa ulaghai wa kifedha na kingono ni jambo la kuwahangaisha sana, na katika mazungumzo yao na Roblox wamehakikisha teknolojia za kuthibitisha umri zitatekelezwa ili kuzuia watu wazima kutumia huduma hiyo.
Kamishna anasema kuwa serikali imewapa majukwaa haya jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba njia za kukwepa hazitumiwi.
Kuna ishara nyingi ambazo sasa zinakusanywa, kama vile vitambulisho vya vifaa. Mnajua mtoa huduma wa mtandao wao ni nani, wanapakua kutoka duka gani la app, na katika hali nyingi, kwa mfano, mkileta simu Marekani na kuipakua kutoka duka la app, wataangalia kipindi cha miezi sita kuona kama kweli wewe ni mkaaji wa Australia. Tumekuwa na mazungumzo makubwa na makampuni kuhusu hili.Bi.Grant
Msemaji wa mawasiliano wa upinzani, Melissa Mcintosh, anasema kuwa hakuna kitu muhimu zaidi kuliko kuwalinda watoto kutokana na madhara ya mitandao ya kijamii.
Anasema kama mama, amekumbana na hili yeye mwenyewe. Lakini anahofia kwamba sheria hiyo haiwezi kutekelezwa na kwamba data ya kibayometriki inaweza kuhatarishwa iwapo mfumo wa Kitambulisho cha Kidigitali utatumika.
Nimekuwa na wasiwasi sana kuwa marufuku hii ya mitandao ya kijamii itafanya kazi, na nimekuwa nikionyesha wasiwasi wangu kwa majuma mengi sasa... Sasa, hatujui ni teknolojia gani ya kuthibitisha umri itakayotumika, na hivyo Waastralia wengi wanawasiliana nami, wakiwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa matumizi ya kitambulisho cha kidigitali.Melissa Mcintosh
Waziri Wells anasema kwamba serikali itakuwa makini katika kufuatilia "mitindo ya kuhamia" ya watumiaji wa mitandao ya kijamii, iwapo watumiaji watajaribu kuepuka marufuku hiyo.
Hata hivyo, Tom Sulston kutoka shirika la haki za kidigitali anahofia kuwa hili litakuwa gumu kudhibiti.
salama wa mtandaoni unashughulika na mitandao kwa kuchagua majukwaa ya pekee mmoja mmoja. Hii haitawahi kuisha kwani watoto na vijana wanazunguka kwenye mtandao wakihamia kwenye majukwaa ambayo bado hawajapigwa marufuku, na majukwaa hayo yanakuwa yasiyo salama zaidi na yasiyo na usimamizi, ambako watoto watakumbana na madhara zaidi kuliko wanavyokutana nayo kwenye majukwaa wanayotumia kwa sasa. Ni vigumu kuamini kwamba Kamishna wa Usalama anaiacha 4Chan, moja ya tovuti zisizo na mpangilio zaidi kwenye Intaneti, iko wazi kwa watoto, huku akifunga milango kwa Reddit, ambayo ina usimamizi na vipengele vya usalama. Kwa kufanya hivi, anasukuma watoto wa Australia kwenye kona za giza zaidi za mtandao ambako hawatakuwa salama zaidi na hawatapata msaada wanapouhitajiTom Sulston





