Taarifa ya Habari 1 Agosti 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese ana enda kuhudhuria tukio kubwa linalo waleta pamoja wa Australia wa Asili katika wilaya ya Kaskazini.


Sherehe ya Garma huandaliwa kila mwaka na hudumu kwa siku nne kuanzia 1-4 Agosti, katika eneo la kanda la kaskazini mashariki la Arnhem Land katika ardhi ya watu wa Yolngu. Shirika la Yothu Yindi Foundation ni mwenyeji wa sherehe hiyo ya Garma, na mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, Denise Bowden, ame eleza shirika la habari la NITV kuwa mwaka huu kuna maadhimisho ya miaka 25 ya tukio hilo.

Wanafunzi wamekaribisha kupitishwa kwa sheria yakupunguza deni ya wanafunzi iliyo pitishwa 31 Julai. Waziri wa Elimu wa Shirikisho Jason Clare amesema kupitishwa kwa muswada huo, kuta saidia walio athiriwa kuokoa kwa wastan $5,500. Mageuzi hayo yata chukua miezi kadhaa kwa ofisi ya ushuru ya Australia kutekeleza, salio za HECS zinatarajiwa kusasishwa kufikia mwisho wa mwaka huu.

Kenya imepinga sheria mpya za biashara na kodi za Tanzania ikizitaja kuwa za kibaguzi na zinazohatarisha ushirikiano wa kiuchumi Afrika Mashariki. Sheria hizo zimewazuia Wakenya kufanya biashara ndogo ndogo Tanzania. Kupitia taarifa rasmi, Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda ya Kenya imeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu amri ya Tanzania iliyoanza kutekelezwa Julai 28, ambayo inawazuia raia wa kigeni kushiriki katika baadhi ya sekta za biashara.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amewashutumu maafisa wa serikali yake kwa kuchangia katika kuliteketeza taifa hilo. Licha ya rais Ndayishimiye kusifiwa kutokomeza machafuko na umwagaji damu ulioshuhudiwa wakati wa utawala wa mtangulizi wake Pierre Nkurunziza, rekodi ya haki za binadamu bado ni mbaya huku udhibiti wa taifa hilo ukisalia mikononi mwa kundi dogo la majenerali wenye nguvu.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service