Watetezi wa wahamiaji na wakimbizi wanasema jamii zilizo katika mazingira magumu, zinapuuzwa katika mwitikio wa serikali kwa athari za kiuchumi za vita katika Mashariki ya Kati.
Nchini Burundi, siku 2 baada ya kutokea milipuko katika kituo kikuu cha kuhifadhi silaha cha jeshi huko Bujumbura, Jeshi lilitangaza idadi rasmi ya awali ya raia 13 waliouawa na wengine 54 kujeruhiwa na wanajeshi watatu waliouawa. Serikali bado haijatoa taarifa.
Nchini Rwanda, kundi la watu 214 wanaohusishwa na makundi ya waasi, ikiwa ni pamoja na FDLR kulingana na mamlaka, wamerejeshwa katika maisha ya kiraia baada ya miezi kadhaa katika kituo walikkokuwa wamekusantwa kwa ajili ya kupewa maadili ya namna ya kuishi upya na raia. Miongoni mwao ni wapiganaji pamoja na raia wanaohusishwa na makundi haya.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.





