Taarifa ya Habari 15 Septemba 2025

Bench - Swahili.jpg

Benki ya ANZ imekiri kujihusisha na mwenendo usiofaa, katika huduma iliyotoa kwa serikali ya Australia, kulingana na Tume ya Uwekezaji na usalama ya Australia (ASIC).


ASIC imesema ANZ ilifeli kuwarejesha hela ilizo dai maelfu ya wateja wake waliofariki na, kupuuza kujibu kwa wakati wapendwa wao walio kuwa wakijaribu kushughulikia mali za wateja walio fariki. Mdhibiti ata omba mahakama ya shirikisho iweke adhabu za $240 million.

Kiongozi wa chama ha Liberal jimboni New South Wales Mark Speakman, amesema ataendelea kutoa ushauri bora wakati, uvumi una sambaa kama washirika wake watafanya mabadiliko ya uongozi. Hali hiyo inajiri wakati chama cha Labor kime shinda kiti kingine katika bunge la jimbo, baada yakushinda eneo bunge la Kiama katika chaguzi dogo iliyo fanyika wikiendi iliyopita.

Nchi ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimejitolea kushirikiana na washirika wengine, wakiwemo Marekani, kuboresha mnyororo wa usambazaji wa madini na kuendeleza mageuzi, wakilenga kuvutia uwekezaji. Kwenye rasimu ya mktababa huo wa kiuchumi iliovujishwa, Kongo na Rwanda zimekubaliana juu ushirikiano wa kiuchumi, ambao ni sehemu ya makubaliano ya amani yaliotiwa siani na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili.

Nyota wa timu ya taifa ya Australia ya mpira wa miguu Matildas Sam Kerr, amerejea uwanjani nakufunga goli baada ya kuwa nje ya mchezo huo kwa miezi 20 kwa sababu ya jeraha. Kerr alifunga goli lake la 100 akichezea Chelsea ya Uingereza. Kerr alipewa fursa yakucheza katika ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Aston Villa, baada yakuto cheza dhidi ya Manchester City.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service