Mwenyekiti wa benki ya ANZ Paul O'Sullivan, ameomba radhi kwa utovu wa nidhamu ya benki hiyo, baada ya benki hiyo kupewa adhabu ya milioni $240. Mweyekiti wa Shirika la Australian Securities and Investments Commission [[ASIC]] Joe Longo, amesema benki ya A-N-Z ime saliti imani yawa Australia, baada ya benki hiyo kukiri ilifanya utovu wa nidhamu kwa kufeli kurejesha hela ilizo dai kwa wateja walio fariki.
Serikali ya Kusini Australia ime thibitisha kifaa cha akili bandia, kita tolewa katika shule za upili za jimbo hilo. Waziri wa Elimu Blair Boyer amesema EdChat, ambayo ni sawa na kifaa cha AI aina ya ChatGPT, kime undwa haswa kwa matumizi ya elimu Kusini Australia na, kime wekewa ulinzi kuwalinda wanafunzi dhidi ya taarifa zinazo dhuru au zisizo faa.
Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Upinzani, CHADEMA, Tundu Lissu yanayohusiana na usikilizwaji wa kesi ya uhaini inayomkabili. Jaji Kiongozi wa kesi hiyo, Dunstan Ndunguru ameahirisha kesi hiyo Jumatatu hadi majira ya saa nane mchana ambapo itasikilizwa katika awamu ya mashtaka.
Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema utoaji chanjo kwa watu walio kwenye hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Ebola umeanza jana Jumapili kusini mwa jimbo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Mlipuko wa ugonjwa huo hatari uliripotiwa mapema mwezi huu kwenye kitongoji cha Bulape na kusababisha vifo vya watu 16 na wengine 68 wanashukiwa kuwa wameambukizwa.