Wazee wa Mataifa ya Kwanza na wanaharakati wa mazingira, wamesema wamesikitishwa na tangazo la malengo ya mazingra ya Waziri Mkuu. Katika mkutano ulio fanyika Garamilla Darwin katika Wilaya ya Kaskazini, kundi hilo lime onya kuwa ukanda wa kaskazini ya Australia ambayo inatarajiwa kukabiliwa na madhara mabaya zaidi ya mabadiliko ya mazingira, umetolewa kama kafara.
Nchini Kenya, mahakama imetoa siku ya Jumanne kibali cha kukamatwa kwa mwanajeshi wa Uingereza. Mwanajeshi huyo anashukiwa kumuua Agnes Wanjiru, mama mwenye umri wa miaka 21 ambaye mwili wake ulipatikana kwenye tanki la maji taka la hoteli ya Nanyuki mnamo mwaka 2012.
Taratibu zinazolenga kumfuta kazi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Vital Kamerhe zinaendelea huku kukishuhudiwa hali ya mfarakano kati ya rais Félix Tshisekedi na mshirika wake huyo wa zamani.