Mkuu wa Shirika la Nishati la Kimataifa amesema akiba ya sasa ya mafuta ya Australia, licha ya kuwa chini ya viwango, si sababu ya kuwa na wasiwasi. Australia ina takriban siku 30 za dizeli zilizo hifadhiwa.
Mvua kubwa iliyosababisha mafuriko nchini Kenya imewaua watu wasiopungua 81 mwezi huu. Hayo ni kwa mujibu wa mamlaka za nchini humo huku mvua ikiendelea kunyesha sehemu nyingi za nchi. Katika eneo la magharibi mwa nchi lililoathiriwa kwa kiasi kikubwa, wakazi walipambana kwenye maji ya mafuriko na kuhamishwa kwenye boti zilizojaa watu. Mafuriko ya ghafla yalifunika vijiji katika kaunti ya Kisumu, na kuharibu takriban ekari 3,000 za mashamba yaliyokuwa na mazao.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mjadala wa mabadiliko ya katiba unaendelea, miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu, suala linaloonekana kuwagawa wanasiasa na wananchi wa taifa hilo. Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wanaona kuwa, mjadala huu sasa unaanza kusababisha kusahaulika kwa masuala muhimu na makubwa yanayoikumba nchi hiyo.
Mshambuliaji wa timu ya taifa Socceroos, Awer Mabil amesema anajiona kwa sasa kama mshauri kwa wachezaji wenzake. Mabil, alikuwa katika kikosi cha Australia cha kombe la dunia miaka nne iliyopita, ame rejeshwa katika timu ya taifa kwa mechi mbili zitakazo chezewa nyumbani kabla ya kombe la dunia mwaka huu.Mabil ambaye ana miaka 26, ame wakilisha Socceroos mara 35. Australia ita cheza dhidi ya Cameroon usiku wa Ijumaa 27 Machi mjini Sydney, kabla yaku kabiliana na Curacao mjini Melbourne, Jumanne ijayo.





