Taarifa ya Habari 23 Septemba 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Waziri Mkuu amesema ombi la utaifa wa Palestina ni fursa ya amani, katika hotuba yake kuhusu soluhu ya nchi mbili, alipo hudhuria kikao cha Umoja wa Mataifa hii leo Jumanne 23 Septemba 2025.


Serikali ya shirikisho ime shtumiwa kwa "kuwafeli wa Australia" kwa kuto kutotekeleza mlinzi wa huduma za simu za dharura kabla ya kupotea kwa matumizi ya hivi karibuni ya Optus. Kukatizwa kwa huduma ya Alhamisi kume ungwa na vifo vinne na ni mara ya pili katika miaka mbili ambapo, kufeli kwa mtandao wa Optus kume maanisa wa Australia hawa wezi tumia huduma ya simu ya dharura.

Msikilizaji mahakama kuu kwenye jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania, hatimaye imepanga tarehe rasmi ya kuanza kusikiliza kesi ya mashtaka ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA na mkosoaji mkubwa wa Serikali, Tundu Lisu. Bw Lisu aliwataja rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, makamu wake, waziri mkuu, mkuu wa jeshi la polisi na yule wa idara ya usalama wa taifa kama sehemu ya mashahidi wake.

Spika wa Bunge la taifa nchini DRC, Vital Kamerhe, amejiuzulu. Alikuwa mada ya ombi ambalo lilipaswa kupigiwa kura wakati wa kikao cha mashauriano katika makao makuu ya Baraza la Wawakilishi mjini Kinshasa. Hatimaye, amewasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa Kongamano la viongozi, ambalo huwaleta pamoja viongozi wa makundi ya wabunge, kulingana na wabunge kutoka chama chake, UNC.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 23 Septemba 2025 | SBS Swahili