Zaidi ya idadi yawa Australia elfu 65 wame tia saini ombi la shirika la Medecins San Frontieres, shirika hilo hujulikana pia kwa Kiingereza kama Doctors Without Borders, au Madaktari wasio na mipaka. Ombi lao lina omba serikali ya shirikisho ifanye mengi zaidi kuingilia swala la Gaza. Seneta wa serikali ya Labor Ed Husic, naye pia amesema serikali ya Australia inahitaji fanya uratibu na vyama vingine kuimarisha vikwazo dhidi ya Israel.
Kuna uwezekano idadi yawa Australia milioni 2.6 wanaweza athiriwa na muswada mpya unao lenga kulinda mishahara ya wafanyakazi wa muda. Waziri wa Ajira Amanda Rishworth anawasilisha sheria bungeni hii leo Alhamisi, kuhakikisha wafanyakazi wanao takiwa fanya kazi wikiendi na zaidi ya masaa yao ya kazi, wana lipwa takriban $40 kwa saa. Kiwango hicho kime hesabiwa na shirika la Fair Work Australia, kulingana na hitaji la saa moja na nusu ya malipo ya kazi ya Jumamosi na kulipwa mshahara mara mbili ukifanya kazi Jumapili.
Kundi la vijana katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, limeanzisha mpango wa kujitolea kurekodi na kutunza kumbukumbu ya vitendo vya uhalifu katika mji huo na viunga vyake. Tangu mwezi Januari mwaka huu, mji wa Goma na maeneo mengine mengi ya mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini yako mikononi mwa waasi wa AFC/M23. Katika ripoti yake iliyochapishwa mapema mwezi huu wa Julai, kundi hilo la vijana limeorodhesha jumla ya visa 47 vya mauaji, visa 75 vya ubakaji, watu 14 waliotekwa na matukio 66 ya uporaji, vyote hivi katika kipindi cha mwezi mmoja.
Nchini Uganda, miezi sita kabla ya uchaguzi wa urais, Rais Yoweri Museveni anajaribu kurejesha udhibiti baada ya mchujo uliogubikwa na vurugu Julai 17 ndani ya chama tawala cha NRM. Uchaguzi huo ulikumbwa na visa vya ghasia na shutuma za udanganyifu katika maeneo kadhaa. Siku ya Jumanne, Julai 22, kwenye mtandao wa kijamii wa X, mkuu wa nchi aliahidi mfululizo wa hatua dhidi ya wale waliohusika, akiahidi "kusafisha" chama chake kutoka kwa wale anaowaita "wabinafsi wanaotumia mamlaka kujinufaishawa."
Mlinzi wa timu ya Melbourne Steven May, amepewa adhabu yakuto cheza mechi tatu zijazo, baada ya kikao cha kamati ya nidhamu ya mchezo wa AFL. Marufuku hiyo ilitolewa kwa tendo lake laku gongana na Francis Evans Jumamosi, kamati hiyo ya watu watatu ilitangaza kuwa May, alistahili punguza kasi yake au ange badilisha mwelekeo wake kwa ajili ya kuepuka au kupunguza athari.