Serikali ya New South Wales imesema wapangaji milioni mbili wanatarajiwa kunufaika na mfumo wa kidijitali wa kuhamisha dhamana yao kati ya nyumba za kupanga. Mfumo mpya wa teknolojia umejaribiwa ili kurahisisha uhamishaji wa kidijitali [[kupitia jukwaa lililopo la Rental Bonds Online]], na kupunguza ucheleweshaji wa kusubiri kurejeshewa dhamana, jambo ambalo linaweza kuwaacha watu bila kuwa na $4,000.
Maafisa bado wanahubiri tahadhari kwa wakazi wa Katherine katika Eneo la Kaskazini, licha ya ishara kwamba huenda wameepuka wimbi la pili la mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga chaki Tropiki cha Narelle. Hapakuwa mvua kubwa usiku kucha, kwa sababu kimbunga hicho cha kitropiki kinaelekea Magharibi mwa Australia.
Chama cha wanasheria nchini Uganda, ULS, kimeishtaki serikali ya Uganda kwa kile chama hicho kimesema polisi kuendelea kuzingira makazi ya mwanasiasa wa upinzani, Robert Kyagulani, maarufu kama Bob Wine. Katika kesi waliyofungua Machi 16, wanasheria wa chama hicho wanavituhumu vikosi vya usalama kuendelea kusigina katiba na sheria za nchi kwa kuzingira makazi ya Bob Wine, tangu kumalizika kwa uchaguzi wa mwezi Januari mwaka huu. Tangu kufanikiwa kuwatoroka polisi baada ya uchaguzi wa Januari 15, polisi wamekuwa wakikataza ndugu, marafiki, viongozi wa chama na hata mawakili kuingia ndani ya nyumba yake, hata kwa kupeleka chakula.





