Muswada mpya unajaribu kutoa kinga kwa wapokeaji wa malipo ya ustawi dhidi ya mfumo wa kinyume cha sheria wa robodebt, kwa kuhitaji ustawi wao kuzingatiwa kabla ya madeni kudaiwa. Chama cha Greens na wabunge wengine wali wasilisha pendekezo hilo jana bungeni, kwa lengo laku tekeleza mapendekezo ya tume yakifalme ambayo bado hayaja takelezwa miaka mbili baadae. Muswada huo utaweka jukuu la utunzaji kwa Idara ya Huduma za Jamii, itaweka kikomo kwa ulipaji wa deni kwa miaka sita na, kupunguza maamuzi yaki elektroniki.
Hali ya kibinadamu katika mji wa El-Fasher nchini Sudan inazidi kuzorota baada ya mashambulizi mapya ya vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) yaliyosababisha vifo, utekaji na uharibifu mkubwa. Madaktari wamesema watu wasiopungua 13, wengi wao wanawake na watoto, waliuawa waliposhambuliwa wakiwa barabarani karibu na mji wa huo mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini. Mtandao wa Madaktari wa Sudan (SDN) umesema mauaji hayo ni sehemu ya kampeni ya mauaji ya kikabila na mauaji ya halaiki yanayolenga raia wasio na silaha katika eneo la Darfur. Kundi hilo limeeleza kuwa miongoni mwa waliouawa walikuwemo watoto watano na wanawake wanne.
Nchini Burundi, Meja Jenerali Bertin Gahungu anashikiliwa na idara za usalama, mamlaka imetangaza. Afisa mkuu wa usalama katika utawala na mkuu wa zamani wa idara ya kijasusi nchini humo, anashtumiwa na mashirika ya haki za binadamu kwa jukumu lake katika ukandamizaji wa maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa rais Nkurunziza mwaka 2015. Kukamatwa katika mazingira yasiyoeleweka, hakujashindwa kuibua hisia. Afisa mkuu aliyenukuliwa na shirika la habari la AFP, anasema kuwa Brigedia Jenerali Bertin Gahungu alikamatwa siku ya Alhamisi, Agosti 21, katika afisi zake na maafisa wa idara ya ujasusi wa Burundi wanaomshikilia kwenye majengo yao.