Mhafidhina maarufu wa chama cha Liberal amekana madai kuwa ana taka wania uongozi wa chama chake, baada ya mfululizo wa machapisho ya uchochezi katika mtandao wa kijamii. Mbunge wa Magharibi Australia Andrew Hastie, ame ongoza kampeni ya hadhara ya sera ya uzalishaji sufuri wa hewa chafu ifutwe na uhamiaji upunguzwe, akisema katika chapisho moja kuwa uhamiaji una stahili laumiwa kwa uhaba wa nyumba nchini.
Serikali ya A-C-T imeweka wazi mipango yakufanya udhibiti kwa nguvu kosa la jinai katika wilaya hiyo. Marisa Paterson ni Waziri wa Kuzuia ukatili wa nyumbani, amesema serikali yake itawasilisha muswada huo kufikia katikati ya mwaka ujao. Ameongezea kuwa anataka hakikisha muswada huo una undwa kwa ushirikiano na wale ambao wame athiriwa zaidi.
Nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda zimekubaliana kuanza utekelezaji wa hatua za kiusalama mwezi ujao chini ya makubaliano yaliyoratibiwa na Marekani. Tangazo hilo limetolewa katika taarifa ya pamoja siku ya Jumatano, katika kile ambacho kitakuwa ni hatua muhimu katika utekelezaji wa makubaliano hayo ya amani huku kukiwa na wasiwasi juu ya maendeleo yake. Makubaliano hayo yaliyofikiwa katika mkutano wa Washington Septemba 17-18na kuripotiwa kwa mara ya kwanza na shirika la habari la Reuters, yataanza Oktoba 1, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja, ambayo pia ilitolewa na Marekani, Qatar, Togo na Kamisheni ya Umoja wa Afrika.
Nchini Uganda, sasa inajulikana Yoweri Museveni atapambana na nani katika uchaguzi wa urais wa mwezi Januari 2026. Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano, Septemba 24, Tume ya Uchaguzi imetangaza kwamba wagombea wanane kati ya 38 wamepasishwa. Miongoni mwao ni rais wa sasa, aliye madarakani tangu mwaka 1986, na mpinzani wake mkuu, mwinamuziki wa zamani Bobi Wine. Kuidhinishwa kwa kugombea kwake hakukuwa na uhakika hadi dakika ya mwisho.