Seneta wa chama cha Liberal Jane Hume amesema Bob Katter lazima aadhibiwe baada ya kutishia kumpiga ngumi mwandishi wa habari. Seneta huyo huru alikuwa aki elezea anavyo unga mkono maandamano ambayo yame zua utata yakupinga uhamiaji, alipo kasirika katika jibu lake kwa swali la mwandishi wa habari wa Chanel 9 Josh Bavas kuhusu asili ya Bw Katter ya Lebanon. Seneta Katter alimkaribia Bw Bavas akiwa ame kunja ngumi, nakumwita mwandishi huyo wa habari mbaguzi wa rangi.
Seneta Amanda Rishworth amewasilisha muswada bungeni, kulinda malipo ya kazi ya masaa ya ziada katika sheria. Wakati vyama vya wafanyakazi vime karibisha hatua hiyo, baadhi ya vikundi vya viwanda vime zua wasiwasi kuhusu muswada huo.
Uzinduzi rasmi wa kampeni za chama tawala cha Mapinduzi CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, umefanyika kwa shamrashamra kubwa katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, mgombea wa urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, alitoa wito kwa Watanzania kushiriki uchaguzi kwa amani na kuwaahidi maendeleo endelevu endapo atapewa dhamana ya kuongoza muhula mwingine.
Rwanda na Msumbiji zimesaini makubaliano ya ‘amani na usalama' wakati rais wa Msumbiji Daniel Chapo alipozuru mji mkuu wa Rwanda, Kigali. Makubaliano hayo yamesainiwa mnamo wakati mashambulizi ya wanamgambo nchini Msumbiji yameongezeka huku vikosi vya nchi hizo mbili vikipambana dhidi ya uasi wa muda mrefu wa wanamgambo, kaskazini mwa Msumbiji.