Bunge wa chama cha Nationals Barnaby Joyce amewasilisha muswada binafsi wakuondoa Australia kutoka lengo la jumla la uzalishaji sufuri wa hewa chafu. Hatua hiyo ina ashiria kuongezeka kwa kikundi cha waufasi wa chama cha Mseto ambao wanapinga uzalishaji sufuri, Baadhi ya wanachama wa Nationals kama Matt Canavan, Colin Boyce, na Michael McCormack pamoja na mbunge wa chama cha Liberal Garth Hamilton wanao taka ahadi hiyo ifutwe.
Waandamanaji wanaopanga maandamano katika daraja maarufu la Sydney Harbour Bridge, Jumapili ijayo 3 Agosti, wamesema wata kabiliana dhidi ya jaribio lolote lakuwazuia. Wanalenga kuelekeza mawazo kwa njaa inayo kabili Gaza ila, Kiongozi wa New South Wales Chris Minns alipinga kwa haraka maandamano hayo, akisema walipata maelezo kuchelewa pamoja na machafuko ya trafiki. Hata hivyo, wanaharakati wamesema daraja hilo ni ishara muhimu linalo wakilisha Australia, na wamesema wako tayari kuchelewesha tukio lao kuambatana na masharti ya usalama.
Watu wasiopungua 21 wameuawa siku ya Jumapili, kufuatia shambulio lililofanywa na waasi wanaoungwa mkono na kundi la itikadi kali linalojiita dola la Kiislamu, IS, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa mujibu wa Dieudonne Duranthabo,ambaye ni mratibu wa shirika la kiraia katika eneo la Komanda, aliyezungumza na shirika la habari la AP, waasi wa ADF mnamo majira ya saa saba usiku walivamia na kushambulia majengo ya kanisa katoliki kwenye eneo la Komanda mashariki mwa Kongo, kuteketeza majumba kadhaa na maduka.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imesema uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika Uchaguzi Mkuu 2025, utafanyika Oktoba 29, mwaka huu, ikibainisha kuwa wapigakura 37,655,559 wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu 2025. Idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 26.55 kutoka milioni 29.7 waliokuwa wamejiandikisha katika daftari mwaka 2020.