Serikali ya Albanese iliwasilisha muswada wa deni ya HECS, waku kata asilimia 20 kutoka deni zilizopo za chuo na TAFE, kama hatua yake ya kwanza ya biashara wiki jana. Sheria hizo zina lenga kupunguza madeni ya wanafunzi, pamoja nakufanya mageuzi kwa mfumo wa malipo.
Muda wausafiri kwa treni bila malipo mjini Sydney, ume ongezwa kwa siku moja hadi asubui ya Jumamosi.Kuanzia leo hadi wikiendi, abiria watatumia huduma za treni na metro mjini Sydney bure, katika hatua yaku kiri miezi ya usumbufu ulio sababishwa na migomo.
Israel iko chini ya shinikizo kuregeza janga lakibinadam linalo endelea Gaza, Canada ikiwa nchi mpya ambayo imechukuwa hatua yakutambua utaifa wa Palestina, na mjumbe wa Marekani akiwa njiani kuelekea Mashariki ya Kati. Mwakilishi huyo wa serikali ya Trump, Steve Witkoff, anatarajiwa kuwasili nchini Israel leo, kwa mazungumzo kuhusu hali inayo endelea Gaza.
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssntenamu, almaarufu kama Bobi Wine amesema mazingira ya kisiasa nchini humo yamekuwa mabaya zaidi kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mapema mwaka 2026. Kwenye mahojiano na shirika la habari la AP kwenye makao makuu ya chama chake cha National Unity Platform, mjini Kampala, Bobi Wine amesema kumekuwa na vitisho dhidi ya maisha yake na wanaharakati wengine wanaohamasisha upinzani dhidi ya rais aliyekaa muda mrefu nchini humo Yoweri Museveni.