Watch FIFA World Cup 2026™ LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Taarifa ya Habari: Serikali yachukua hatua yakupunguza bei ya mafuta nchini baada ya siku kadhaa za shinikizo

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Waziri Mkuu amesema serikali yake imechukua hatua ya kupunguza bei ya mafuta kote nchini, kwa sababu hata kama vita vitaisha mara moja, madhara ya kiuchumi yataendelea.


Serikali inapunguza ushuru wa mafuta kwa nusu, jambo ambalo litawaokoa watumiaji senti 26 kwa lita kwa petroli na dizeli, na kupunguza gharama kwa makampuni ya malori kwa senti 34 kwa lita. Hatua hizo zitagharimu zaidi ya dola bilioni mbili na nusu.

Mazishi ya Rhoda Roberts A-O yatafanyika katika Kanisa Kuu la St Carthage huko Lismore, katika Nchi yake mpendwa ya Bundjalung. Akiwa mwanamke mwenye fahari Widjabul Wieybal kutoka Taifa la Bundjalung, Rhoda anakumbukwa kama mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa wa sekta ya sanaa na ubunifu nchini Australia.

Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC, kuanzia leo inazindua zoezi endelevu la kujiadikisha kwa wapiga kura wapya wapatao zaidi ya Milioni 2.5 kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Mwenyekiti wa Tume hiyo Erustus Ethekon, amesema zoezi hilo litafayika nchi nzima na wanaolengwa ni vijana ambao hawajawahi kupiga kura. Katika mchakato huu, Tume hiyo inasema, zoezi hili linaondoka kwenye maeneo bunge kwenda mitaani na vijijini ili kuwapata wapiga kura wapya.


Share

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now