Miaka mitano ya uhai wa bunge la 12 la Tanzania, ulitamatika Jumapili ya wikendi iliopita kufuatia tangazo la rais Samia Suluhu Hassan, kulivunja bunge hilo kwa mujibu wa katiba. Kuvunjwa kwa bunge hilo kunafungua ukurasa mwingine kwa vyama vya siasa kuanza kuteua wagombea wa nafasi za ubunge kuelekea uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu.
Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imepata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye mechi yao ya ufunguzi ya Kundi A iliyochezwa kwenye uwanja wa Moi Kasarani, jijini Nairobi. Rais William Ruto amewaahidi wachezaji wa Harambee Stars shilingi milioni 600 iwapo timu hiyo itachukua ubingwa wa CHAN mwaka huu, pamoja na shilingi milioni moja kwa kila mchezaji kwa kila ushindi wa mechi katika michuano hiyo.