Taarifa ya Habari 9 Septemba 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Dau Akouny, mmoja wa wavulana wawili walio uawa katika shambulizi la kisu mjini Melbourne wikiendi iliyopita, amekumbukwa na familia yake kama "mtoto mzuri" na alikuwa "sehemu ya mustakabali wa kesho wa jumuiya."


Kiongozi wa upinzain Sussan Ley amesisitiza ujumbe wa ushikamano kwa jumuiya ya wahindi wa Australia, wakati amesema anajutia madai kuhusu majasusi wa kichina yaliyo tolewa na Seneta wa chama cha Liberal wakati wa uchaguzi wa shirikisho.

Katika jimbo la New South Wales, fukwe kadhaa zimefungwa baada ya papa mweupe kutambuliwa karibu ya fukwe hiyo, kufuatia shambulizi lililo sababisha kifo la mtu aliyekuwa akifanya mchezo wakutereza juu ya maji karibu ya fukwe hiyo.

Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA Tundu Lissu, Jumatatu amepandishwa kwa mara ya kwanza kwenye Mahakama Kuu kunakosikilizwa kesi ya uhaini inayomkabili. Kesi hiyo hata hivyo imesogezwa mbele hadi Septemba 9, baada ya mvutano mkubwa wa kisheria ulioibuka kuhusu kuahirishwa mara kwa mara kwa kesi hiyo.

Hali ya wasiwasi bado inashuhudiwa Uvira, jimboni Kivu Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa siku ya sita mfululizo mji huo ulisalia mahame. Wapiganaji wa Wazalendo, wanataka serikali jijini Kinshasa, kumwondoa Jenerali Olivier Gasita, aliyetumwa katika eneo himo kwa madai kuwa, ana ushirikiano wa karibu na waasi wa AFC/M23 kwa kile anachoelezwa kuwa ni kutoka kwa jamii ya Banyamulenge.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 9 Septemba 2025 | SBS Swahili