Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Taarifa ya Habari: Akiba itazidi matumizi na kodi katika bajeti ijayo Mweka Hazina aeleza taifa

Bench - Swahili.jpg

Mweka Hazina Jim Chalmers amesema bajeti ya shirikisho ya wiki ijayo itakuwa na kikomo chake kikubwa zaidi, wakati akiba ikitarajiwa kuzidi mabadiliko ya matumizi na kodi.


Bw. Chalmers ame ongezea kuwa mkakati wa fedha wa bajeti utaendeshwa hasa na akiba, badala ya mabadiliko ya kodi.

Waziri Mkuu wa Japani Sanae Takaichi, amewasili nchini Australia kwa ziara yake ya kwanza kama kiongozi wa taifa hilo.

Bi. Takaichi atakutana na Waziri Mkuu Anthony Albanese mjini Canberra ambako mkutano wao unatarajiwa kuzingatia makubaliano muhimu ya madini na uhakika kuhusu usambazaji wa gesi.

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, MSF, limeonya kuwa mashambulizi dhidi ya wahudumu na vituo vya afya yanaendelea kushuhudiwa katika maeneo yenye migogoro licha ya ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kuwalinda. Onyo hilo limetolewa Jumapili, katika maadhimisho ya miaka 10 tangu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifalilipopitisha Azimio la kuwalinda wahudumu wa afya, misaada ya kiutu, miundombinu, usafiri na vifaa vya matibabu wakati wa vita.

Kocha mstaafu wa Manchester United Sir Alex Ferguson, amelazwa hospitalini nchini Uingereza. Sir Alex alipelekwa hospitalini kutoka uwanja wa Old Trafford kwa gari la wagonjwa, saa moja kabla ya kuanza kwa mechi ya timu yake ya zamani dhidi ya watani wao Liverpool FC.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa zaidi.


Share

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now