Watch FIFA World Cup 2026™ LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Taarifa ya Habari: Australia haishiriki katika vita dhidi ya Iran, Waziri wa Ulinzi aeleza vyombo vya habari

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Waziri wa Ulinzi Richard Marles amethibitisha kwamba Australia haishiriki katika hatua za kijeshi zinazoendelea dhidi ya Iran.


Serikali ya Australia iko chini ya shinikizo la kutafuta njia ya kuwarejesha nyumbani raia waliokwama ng'ambo katika mgogoro unaoendelea wa Mashariki ya Kati. Maseneta wa chama cha Liberal wameitaka Idara ya Mambo ya Nje iidhinishe matumizi ya ndege za kijeshi, kwa ajili ya kuwarejesha nyumbani, lakini Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong amesema hilo halitawezekana wakati anga zikiwa zimefungwa.

Uwanja wa ndege wa Bangboka huko Kisangani, kaskazini mashariki mwa DRC, umelengwa tea na ndege zisizo na rubani mnamo Machi 1, 2026, mwezi mmoja baada ya shambulio lingine. Hakukuwa na uharibifu mkubwa wa vifaa, lakini kulikuwa na watu waliohama katika eneo linalozunguka uwanja huo. Mamlaka ya mkoa inaishutumu kundi lenye silaha la AFC/M23 na Rwanda.

Nchini Burkina Faso,milipuko ilisikika karibu na makaazi ya rais jijini Ouagadougou, mwishoni mwa wiki iliyopita na kuzua wasiwasi wa kuwepo kwa jaribio la kumpindua kiongozi wa jeshi Ibrahim Traore. Milio hiyo ilizua wasiwasi katika jiji hilo, kabla ya serikali kutoa taarifa na kueleza kuwa, magari sita yaliyokuwa na vilipuzi ndio yaliyolipuka karibu na makaazi ya rais.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.


Share

Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now